Ruto: Kulikuwepo njama ya kumteka mwenyekiti wa uchaguzi
Nchini Kenya, rais William Ruto, amedai kuwa, kulikuwa na mpango wa kumteka na kumuua, Mwenyekiti wa uchaguzi Wafula Chebukati, ili kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa urais, wakati wa uchaguzi mkuu, mwaka uliopita.
Imechapishwa:
Cheza - 00:28
Ruto ametoa madai hayo katika kikao na Makamishena wa Tume huru, akiwemo Chebukati ambaye muda wake kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi umefika mwisho.
“Tunafahamu kwamba kulikuwepo na njama ya kumteka na kumuua Chebukati.” Ameeleza rais Ruto.
Madai haya ya Ruto, yamelaaniwa na wanasiasa wa upinzani, wanaosema ni shutuma zisizokuwa na ushahidi wowote.
Muungano wa Azimio la Umoja, umeendelea kusisitiza kuwa waliibiwa kura katika uchaguzi huo.