Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Muda wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wakamilika

Msikilizaji nchini Kenya, hivi leo ndio muda wa mwisho kuwa madarakani kwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati, pamoja na makamishna wengine wawili kati ya 7, hatua ambayo inaacha pengo la uongozi kwenye tume hiyo.

Wafula Chebukati, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini kenya anayeondoka
Wafula Chebukati, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini kenya anayeondoka REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Ni miaka sita ambayo haikuwa rahisi kwa tume hiyo hasa katika uchaguzi wa mwaka 2017 na ule wa Agosti mwaka jana.

Wanasheria wanamtazamo gani? Carol Korir, amezungumzwa na Steve Oguttu, mtaalamu wa masuala ya utawala akiwa Kenya.

β€œNafasi ya mwenyekiti ambaye muda wake umekamilika itatangazwa ili watu watume maombi ya kujaza nafasi yake.” amesema Steve Oguttu.

Chebukati amekuwa akituhumiwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, rais Ruto akimsifia mwenyekiti wa kutangaza matokeo kulinagana na walivyopiga kura raia wa kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.