Pata taarifa kuu
BURKINA FASO - UFARANSA -MAENDELEO

Ufaransa kuendelea kushirikiana na Burkina Faso katika vita dhidi ya wanajihadi

Serikali ya Ufaransa, imesema itaendelea kushirikiana na kuisaidia nchi ya Burkina Faso katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi na kwamba ina Imani uhusiano utaendelea kusalia licha ya mvutano wa kidiplomasia.

Chrysoula Zacharopoulou, waziri anayehusika na maendeleo, ushirikiano wa kimataifa na Francophone
Chrysoula Zacharopoulou, waziri anayehusika na maendeleo, ushirikiano wa kimataifa na Francophone © Vincent Fournier/Jeune Afrique
Matangazo ya kibiashara

Uhusiano baina ya nchi hizi mbili ulizorota zaidi wiki iliyopita baada ya serikali ya Ouagadogou, kutaka balozi wa ufaransa aliyeko aondolewe.

Chrysoula Zacharopoulou ni waziri anayehusika na maendeleo, ushirikiano wa kimataifa na Francophone.

“Nimekuja kuwaletea ujumbe ulio wazi unaohusu kuendelea kuimarika kwa uhusiano wa nchi yangu, Ufaransa itaendelea kujitolea katika nyanja zote, kiafya, kiusalama na kimaendeleo.”amesema Chrysoula Zacharopoulou.

Burkina Faso imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya makundi ya wanajiahadi wanaoendelea kusumbua utulivu wa katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo kwa muda mrefu sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.