Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Watu 30 watekwa nyara na watu wenye silaha katika kituo cha treni nchini Nigeria

Watu wenye silaha wameteka nyara zaidi ya watu 30 wakati wa shambulio kwenye kituo cha treni kusini mwa Nigeria, polisi na mamlaka za mitaa zimesema siku ya Jumatatu. Utekaji nyara ni jambo la kawaida nchini Nigeria, hasa katika majimbo ya kaskazini magharibi na kati.

Shambulio la kituo cha treni katika jimbo la Edo lilitokea Jumamosi usiku, kulingana na polisi na mamlaka za mitaa. Washambuliaji walifyatua risasi kabla ya kuwateka nyara abiria waliokuwa wakisubiri treni kuelekea Warri, kusini zaidi, kulingana na vyanzo hivyo.
Shambulio la kituo cha treni katika jimbo la Edo lilitokea Jumamosi usiku, kulingana na polisi na mamlaka za mitaa. Washambuliaji walifyatua risasi kabla ya kuwateka nyara abiria waliokuwa wakisubiri treni kuelekea Warri, kusini zaidi, kulingana na vyanzo hivyo. © AP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Machi 2022, watu wenye silaha walilipua sehemu ya njia ya reli kati ya mji mkuu, Abuja na Kaduna (kaskazini), na kuua watu wanane na kuwateka nyara makumi ya abiria, walioachiliwa kwa miezi iliyofuata kwa fidia.

Shambulio la kituo cha treni katika jimbo la Edo lilitokea Jumamosi usiku, kulingana na polisi na mamlaka za mitaa. Washambuliaji walifyatua risasi kabla ya kuwateka nyara abiria waliokuwa wakisubiri treni kuelekea Warri, kusini zaidi, kulingana na vyanzo hivyo.

Afisa Habari wa Jimbo la Edo Chris Nehikhare ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu 32 walitekwa nyara lakini mmoja wao alifanikiwa kutoroka. Polisi na wawindaji wa eneo hilo walianza kuwasaka watekaji nyara, ameongeza. "Tumezingira eneo hili. Tunajua misitu kuliko wao," amehakikishia Bw. Nehikhare.

Mwishoni mwa mwezi wa Februari, Wanigeria watamchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani ambaye hatawania tena tena baada ya mihula miwili, huku, nchi yake ikiwa katika mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukosefu wa usalama kamili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.