Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Rais Ruto atetea hatua ya serikali yake kuhalalisha GMO

Rais wa Kenya, William Ruto kwenye mahojiano na vyombo vya Habari nchini humo, ametetea mapendekezo yake bungeni, kutaka mabadiliko ya katiba ili kurejeshwa kwa ofisi ya kiongozi wa upinzani, na kukanusha madai kuwa anafanya hivyo ili kumpa kazi mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

“Wale wote waelewe mimi simtafutii mtu kazi, nimeona kiongozi wa upinzani akisema yeye hataki hiyo kazi, Nani alisema mimi natafutia mtu kazi?” amesisitiza rais Ruto

Aidha, Ruto ametetea uamuzi wa serikali yake kuagiza mahindi yaliyozalishwa Kisayansi maarufu kama GMO ili kusaidia kupambana na ongezeko la kupanda kwa gharama ya maisha na kukanusha ripoti kuwa ni hatari kwa matumizi.

“Mimi kama kiongozi wa nchi siwezi kuhatarisha masiha ya watu walionichgua, umesikia mtu amemea pemebe huko Afrika kusini kwa sababu amekula GMO?” Ametilia mkazo rais Ruto.

Rais wa Kenya, William Ruto akijiu maswali ya wanahabari nchini humo, katika Ikulu ya Nairobi, usiku wa kuamkia leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.