Pata taarifa kuu
TANZANIA-SIASA-UONGOZI

CHADEMA: Tumelipokea kwa tahadhari kubwa tangazo la rais Samia

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,hapo Jumanne, ametangaza kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, iliyopigwa marufuku miaka sita iliyopita na mtangulizi wake Hayati John Magufuli. Hatua hii inakuja baada ya rais Samia kukutana na wanasiasa wa upinzani wiki hii.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Freeman Mbowe
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Freeman Mbowe tabelltz.com
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Freeman Mbowe, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, amesema wao kama wapinzani, wanakaribisha hatua hiyo, lakini wanaipokea kwa tahadhari.

“Tamko la Rais tumelipokea kwa mtazamo chanya lakini kwa tahadhari kubwa. Taifa letu limekuwa na mfumo wa ukandamizaji wa demokrasia kwa muda mrefu kuanzia ngazi ya taifa mpaka ngazi ya Vitongoji na kwenye Serikali za Mitaa.”amesema Mbowe.

Mbali na mikutano ya hadhara na katiba mpya, rais Samia pia alitangaza kuendelea kwa mchakato wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa na tume ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.