Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya : Muungano wa kisiasa wa azimio wake Odinga huenda ukasambaratika

Hofu ya kutokea mpasuko ndani ya muungano wa kisiasa wa upinzani nchini Kenya, Azimio, inazidi kuongezeka wakati huu rais wa zamani Uhuru Kenyatta, akitarajiwa kuachia ngazi kama kiongozi wa muungano huo.

Kinara wa muungano wa Azimio nchini Kenya Raila Odinga na aliyekuwa mgombea mwenza wake Martha Karua
Kinara wa muungano wa Azimio nchini Kenya Raila Odinga na aliyekuwa mgombea mwenza wake Martha Karua AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na mvutano kuhusu mrithi wake n ahata mtu atakayepewa nafasi ya kupeperusha bendera ya muungano huo katika uchaguzi ujao wa rais, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wote wakionesha nia.

Wachambuzi wa siasa wanaitazamaje hali hii? Torosterd Alenga, anaangazia hili akiwa Nairobi nchini Kenya.

“Swala la mpasuko huo lilikuwa ni lini litafanyika, nadhani kiongozi wa muungano huo atasalia kuwa Raila Odinga”ameelezaTorosterd Alenga

Odinga alikuwa anaungwa mkono na rais wa zamani Uhuru Kenyatta kumrithi katika uchaguzi mwa mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.