Pata taarifa kuu
DRC- SIASA

DRC: CENI imeanzisha zoezi la kuwatambua na kuwaandikisha wapiga kura

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, CENI, imeanza zoezi la kuwatambua na kuwaandikisha wapiga kura, kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Desemba mwaka 2023. 

Ofisi ya tume ya uchaguzi nchini DRC Jijini Kinshasa
Ofisi ya tume ya uchaguzi nchini DRC Jijini Kinshasa Daniel Finnan
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hilo limeanzia katika mikoa 10 ikiwemo ile ya Kongo-central, Kinshasa, Kwango, Kwilu, Mai-ndombe miongoni mwa mingine. 

Tume ya Uchaguzi inasema wapiga kura wanatakiwa kujaza taarifa zao muhimu kuwatambua lakini pia kufahamu wanakotokea.

CENI inasema inatarajiwa kuwaandikisha wapiga kura Milioni 20 katika mikoa hiyo ambayo zoezi hilo limengo’a nanga siku ya Jumamosi. 

Zoezi hilo, linatarajiwa kuendelea katika mikoa hiyo kwa siku 30 zijazo kabla halijahamia katika maeneo mengine. 

Tume hiyo ya Uchaguzi inatoa wito kwa wapiga kura wapya kujitokeza kwa wingi badala ya kusubiri mpaka siku za mwisho, huku kila raia wa nchi hiyo, aliye na umri wa miaka 18 na kuendelea akihamasishwa kujitokeza. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.