Afrika Kusini: Tisa wafariki katika mlipuko wa lori la gesi karibu na Johannesburg
Watu tisa wamefariki na wengine karibu 40 kujeruhiwa katika mlipuko wa lori la gesi huko Boksburg, yapata kilomita 40 mashariki mwa Johannesburg, maafisa walisema Jumamosi.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Lori hilo lilikwama chini ya daraja, karibu na hospitali, lakini pia kwenye makaazi ya watu Jumamosi asubuhi.
"Wazima moto waliingilia kati, lakini kwa bahati mbaya lori lililipuka," William Ntladi, msemaji wa idara ya huduma za dharura katika eneo hili, ameliambia shirika la habari la AFP.