Pata taarifa kuu

ECOWAS yafafanua mradi wake wa kikosi kipya cha kupambana na ugaidi na mapinduzi

Wakuu wa majeshi wa nchi za jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS walikutana mjini Bissau siku ya Jumatatu. Mwishoni mwa mkutano huo, walielezea chaguzi mbili zinazowezekana za kukabiliana na ugaidi na mapinduzi ya kijeshi, na kuangazia matatizo fulani ya kiuchumi na kisiasa.

Bendera za nchi wanachama wa ECOWAS wakati wa mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo mjini Accra, Ghana, Februari 3, 2022.
Bendera za nchi wanachama wa ECOWAS wakati wa mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo mjini Accra, Ghana, Februari 3, 2022. AFP - NIPAH DENNIS
Matangazo ya kibiashara

Wakikutana mjini Bissau mnamo Jumatatu, Desemba 19, Wakuu wa majeshi wa nchi za ECOWAS walitoa maelezo kuhusu mradi wao wa kikosi kipya cha kupambana na ugaidi. Chaguzi mbili ziliwasilishwa.

Chaguo la kwanza n la uwezo mkubwa na nguvu za kutosha. Kikosi kipya cha kikanda cha kukabiliana na ugaidi kitakuwa na "misheni ya kufanya mashambulizi na uharibifu, ulinzi wa raia na ulinzi wa" miundombinu muhimu". Lakini Wakuu wa majeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanaeleza kwamba pendekezo hili "lina matatizo ya kisiasa", kuanzia "kukubalika kwake na nchi mwenyeji" na "mtazamo wa maoni ya umma".

Ni wazi kwamba, kikosi hiki, ambacho haki zake zitakuwa sawa na za kikosi cha zamani cha Ufaransa cha Barkhane katika ukanda wa Sahel, ambacho kina hatari ya kutokaribishwa vema na baadhi ya nchi wanachama, na hasa miongoni mwa zile zinzohusika kwanza na tishio la kigaidi la wanajihadi. Hakuna haja ya kutoa mfano wa Mali, taarifa kwa vyombo vya habari ya ECOWAS inaikwepa kwa uangalifu. Hata hivyo, inaonekana kuwa chaguo hili pia linatoa "vikwazo muhimu vya kifedha" na kwamba "ufanisi wake wa muda mrefu haukuzingatiwa".

Mali, Burkina na Guinea, hazikushiriki mkutano

Mbali na mapambano dhidi ya ugaidi, mamlaka ya kikosi kipya cha kikanda pia yanastahili kujumuisha kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba, iwapo kutatokea mapinduzi. Wakuu wa majeshi wa ECOWAS wanabainisha kwa kwamba hii itakuwa "uingiliaji kati changamano" na kwamba "utekelezaji wake unaweza kuwa mgumu", "hasa ​​wakati watu na/au sehemu kubwa ya vikosi vya kijeshi vinaunga mkono 'mapinduzi husika.

Mali, Burkina na Guinea, chini ya vikwazo vya ECOWAS, kutokana na mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni, hazikuwepo katika mkutano huu. Wakuu wa majeshi wa nchi za Afrika Magharibi wanapendekeza kwamba waweze kushiriki katika majadiliano yajayo "kuhusiana na masuala ya usalama".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.