Pata taarifa kuu

Ujerumani yarejeshea Nigeria shaba 22 zilizoibwa kutoka kwa Ufalme wa Benin

Ujerumani imeirejesha Nigeria shaba 22 za ufalme wa zamani wa Benin, ziliporwa wakati wa ukoloni, wakati wa sherehe rasmi mjini Abuja siku ya Jumanne.

Makubaliano yalihitimishwa mnamo Julai 1 kati ya Berlin na serikali ya Nigeria baada ya miaka mingi ya mazungumzo ya kurejesha kazi ambayo inasambazwa katika makumbusho ishirini ya Ujerumani.
Makubaliano yalihitimishwa mnamo Julai 1 kati ya Berlin na serikali ya Nigeria baada ya miaka mingi ya mazungumzo ya kurejesha kazi ambayo inasambazwa katika makumbusho ishirini ya Ujerumani. via REUTERS - Horniman Museum and Gardens
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesafiri hadi mji mkuu wa Nigeria kukabidhi kibinafsi vitu 22, ambavyo ni pamoja na vichwa vilivyotengenezwa kwa shaba na kazi zingine. "Tunachorudisha ni sehemu ya historia yenu, tunachorudisha ni sehemu ya jinsi mlivyo," Waziri Baerbock amesema kwenye sherehe hiyo. "Tuko hapa kurekebisha kosa," ameongeza.

Waziri wa Utamaduni wa Nigeria Lai Mohammed amepongeza urejeshaji huu wa kwanza, akiishukuru Ujerumani hasa kwa "ushirikiano" wake. Pia ametoa wito kwa mataifa mengine na majumba ya makumbusho ambayo bado yanashikilia vitu vya kale vya Nigeria 'kuvitoa', akisisitiza kwamba kazi hizi ni 'utamaduni wetu na urithi wetu', kwamba zina 'mahali' yao nchini Nigeria na hakuna mahali pengine.

Makubaliano yalihitimishwa mnamo Julai 1 kati ya Berlin na serikali ya Nigeria baada ya miaka mingi ya mazungumzo ya kurejesha kazi ambayo inasambazwa katika makumbusho ishirini ya Ujerumani. Makumbusho yanayohusika na urejeshaji huu ni ya Linden huko Stuttgart (kusini), ya Grassi huko Leipzig (mashariki), MARKK huko Hamburg (kaskazini), makumbusho ya Rauten-Joest huko Cologne (magharibi), pamoja na Makumbusho ya Ethnological ya Berlin .

Jumba la Makumbusho la Ethnological la Berlin pekee lina vitu 530 vya kihistoria kutoka kwa ufalme wa zamani wa Benin, ikiwa ni pamoja na shaba 440, zinazozingatiwa kuwa mkusanyiko muhimu zaidi baada ya ule wa Makumbusho ya Uingereza huko London. Mpango huu ni sehemu ya mfululizo wa hatua zilizochukuliwa na Ujerumani hivi majuzi kujaribu kuchukulia uhalifu wa wakati wa ukoloni, kama vile kutambuliwa rasmi Mei 2021 kwa mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa nchini Namibia.

Shaba hizo, ambazo ni miongoni mwa kazi maarufu za Kiafrika, ziliporwa kutoka kwa ufalme wa kale wa Benin, kusini mwa Nigeria. Nyingi ziliporwa katika mwaka 1897, wakati msafara wa Waingereza uliposhambulia na kuharibu jiji la Benin (sasa kusini mwa Nigeria), na kuiba maelfu ya michongo ya pembe za ndovu na chuma katika kupita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.