Pata taarifa kuu

Msafara wa kwanza wa msaada wa chakula wa UN kuelekea Tigray tangu kusitishwa kwa mapigano

Msafara wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ulmeingia katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia siku ya Jumatano, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kusainiwa mapema mwezi Novemba kwa makubaliano ya kumaliza mzozo wa miaka miwili kaskazini mwa Ethiopia, serikali imesema.

Msafara magari ya shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umeingia katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia siku ya Jumatano, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kutiwa saini mapema mwezi Novemba.
Msafara magari ya shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umeingia katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia siku ya Jumatano, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kutiwa saini mapema mwezi Novemba. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na WFP, msafara huu ulipitia jimbo jirani la Amhara. Njia hii ilikuwa haijatumika tangu mashambulizi ya waasi kutoka Tigray mnamo mwezi Juni 2021.

Vikosi vya Amhara na wanamgambo, ambao wanaunga mkono jeshi la shirikisho la Ethiopia dhidi ya waasi wa Tigray, hadi sasa wamekataa kupitishwa kwa msaada kwa Tigray, kulingana na vyanzo vya kibinadamu.

"Msafara wa WFP ndio kwanza umeingia Tigray kupitia ukanda wa Gondar (mji wa Amhara kilomita 180 kutoka Tigray), kwa mara ya kwanza tangu mwezi Juni 2021," limesema shirika la Umoja wa Mataifa.

Msafara wa lori 15 ni shehena ya kwanza ya WFP kuingia Tigray tangu makubaliano ya amani yaliyotiwa saini Novemba 2 mjini Pretoria na serikali ya Ethiopia na mamlaka ya waasi huko Tigray, Claire Nevill, afisa wa usalama ameliambia shirika la habari la AFP.

"Msaada muhimu wa chakula sasa utasambazwa katika siku zijazo kwa wakazi wa eneo la Mai Tsebri", lililoko takriban kilomita 30 katika jimbo la Tigray, imeongeza WFP, na "chakula na vifaa vya matibabu vitafuata kwa haraka, kupitia njia zote zinazowezekana. "

Viongozi wa kijeshi kutoka pande zote mbili siku ya Jumamosi walitia saini waraka wa utekelezaji wa mpango huo, ikiwa ni pamoja na kuwapokonya silaha waasi, kurejesha huduma na "bila kuzuiliwa" utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa Tigray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.