Pata taarifa kuu

Jenerali wa Mali Gamou atoa wito kwa vijana wa Tuareg kukusanyika Gao kupigana na EIGS

El Hadj Ag Gamou, jenerali wa jeshi la Mali na mtu muhimu wa kundi la kujihami la jamii yaTuareg kutoka kabila la Imghmad ametoa wito kwa vijana wa Kituareg kutoka Mali na nje ya nchi hiyo kwenda Gao haraka kuulinda mji huo dhidi ya wanajihadi wa kundi la Islamic State katika Sahara Kubwa (EIGS).

Jenerali El Hadj Ag Gamou, mjini Gao mnamo mwaka wa 2013.
Jenerali El Hadj Ag Gamou, mjini Gao mnamo mwaka wa 2013. SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa lugha ya Kituareg ya Tamasheq, iliyosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, Jenerali El Hadj Ag Gamou amewaalika vijana kutoka jamii yake wanaoishi ndani na nje ya Mali wanaojua kushika silaha kujikusanya sehemu mmoja kwa lengo la kulinda ardhi zao.

'Pepo mbaya ambaye lameanza kukita mizizi katika eneo hili' 

"Ni ujumbe ambao unashirikiwa na wahusika wote muhimu wa Kaskazini, wawe wanatoka katika kundi letu au hata viongozi wengine wa kimila na kisiasa, kwa sababu kuna pepo ambaye ameanza kukita mizizi katika mkoa huu ambaye kuna hatari ya kukumba vyote atakavyokutana navyo, ikiwa ni pamoja na watu na mali,” anaelezea Moussa Acharatoumane, kiongozi wa kundi 

 wapiganaji la Movement for the Salvation of Azawad (MSA), mshirika wa Jenerali Gamou kwenye uwanja wa mapigano.

Amesema pepo akimaanisha kundi la wanajihadi wa Islamic State katika Sahara Kubwa (EIGS). Kundi hili, ambalo lilitangaza kuungana na kundi la Islamic State, linataka kudhibiti eneo la kaskazini mwa Mali na kuunda ukhalifa, vyanzo kadhaa vimeongeza. Hata hivyo, Jenerali huyo wa Mali hasemi kwa sasa msimamo wake utakuwaje kuhusiana na wanajihadi wa kundi linalotetea Uislamu na Waislamu, ambao pia wametangazwa kuwa wapinzani wa kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.