Pata taarifa kuu

ICC yaamuru waathiriwa wa machafuko yaliyochochewa na kundi la Ntaganda kufidiwa

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ICC imeamuru ifanyike tathmini ya fidia kwa wahathiriwa wa uhalifu unaodaiwa ulifanyika na wafuasi wa mbabe wa kivita wa DR Congo Bosco Ntaganda.

Bosco Ntaganda, wakati wa sherehe za kuingizwa kwa wapiganaji wa waasi katika jeshi la DRC, Januari 2009 huko Kivu Kaskazini.
Bosco Ntaganda, wakati wa sherehe za kuingizwa kwa wapiganaji wa waasi katika jeshi la DRC, Januari 2009 huko Kivu Kaskazini. AFP PHOTO/Walter ASTRADA
Matangazo ya kibiashara

Ntaganda, ambaye alipewa jina la bandia "Terminator", alipatikana na makosa 18 mkiwemo ubakaji, utumwa wa ngono , na kuwatumikisha watoto kama wanajeshi.

Mwaka 2019 Alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Kimataifa ya jinai kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanyika mashariki mwa DRC mwaka 2002 na 2003,

Baada ya miezi kumi na minane iliyopita, chumba cha mahakama kimetathmini kiasi cha uharibifu uliosababishwa na kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Patriotic Front for the Liberation of Congo kwa dola milioni 30... huku jopo la majaji wanaofuatilia rufaa likiiwataka majaji kuhakiki nakala iliyokuwa imetolewa hapo awali na kusema kiwango cha fidia hiyo ni kukubwa mno.

Ntaganda ambaye alizaliwa nchini Rwanda mwenye umri wa miaka 46-muasi wa zamani amekuwa akihusika na mizozo mbali mbali ya kivita nchini Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.