Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Watano wauawa katika shambulizi dhidi ya msafara wa seneta wa Nigeria

Watu watano waliuawa Jumapili katika shambulizi dhidi ya msafara uliokuwa umembeba seneta wa upinzani kusini mashariki mwa Nigeria, eneo lililokumbwa na ghasia na mvutano wa watu wanaotaka kujitenga kwa eneo lao, polisi imesema siku ya Jumatatu.

Mashambulizi kama hayo yameua zaidi ya polisi 100 na vikosi vingine vya usalama katika eneo hilo tangu mwanzoni m wa mwaka huu, kulingana na hesabu za vyombo vya habari nchini humo.
Mashambulizi kama hayo yameua zaidi ya polisi 100 na vikosi vingine vya usalama katika eneo hilo tangu mwanzoni m wa mwaka huu, kulingana na hesabu za vyombo vya habari nchini humo. © Goran Tomasevic Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watu wenye silaha walifyatua risasi siku ya Jumapili kwenye msafara wa magari ya Ifeanyi Ubah, seneta kutoka chama cha upinzani cha Young Progressives Party, katika Jimbo la Anambra.

"Maafisa wawili wa polisi waliokuwa wamemsindikiza, wasaidizi wake wawili wa kiraia na mtu mpita njia mmoja waliuawa katika shambulio hilo," msemaji wa polisi wa jimbo hilo Tochukwu Ikenga ameliambia shirika la habari la AFP. Maafisa wengine wawili wa polisi walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini, ameongeza.

Seneta huyo alitoka "bila kujeruhiwa", amesema, akiongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kuwapata washambuliaji na kubaini nia yao.

Shambulio hili, lililotokea miezi mitano kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge, halikudaiwa na kundi lolote.

Eneo la Kusini-mashariki mwa Nigeria linakabiliwa na hali ya kuongezeka kwa ghasia, zinazolaumiwa na mamlaka juu ya vuguvugu llialodai Uhuru kwa wakazi wa Biafra (IPOB). IPOB, ambayo inataka kuanzishwa kwa jimbo tofauti kwa kabila la Igbo, imekanusha mara kwa mara kuhusika na ghasia hizo.

Mashambulizi kama hayo yameua zaidi ya polisi 100 na vikosi vingine vya usalama katika eneo hilo tangu mwanzoni m wa mwaka huu, kulingana na hesabu za vyombo vya habari nchini humo.

Magereza pia yalivamiwa, na kuwezesha wafungwa wengi kutoroka na visa vingi vya wizi wa silaha, kama vile ofisi za tume ya kitaifa ya uchaguzi.

Kiongozi wa IPOB, Nnamdi Kanu, amefungwa na serikali na kushtakiwa kwa uhaini, baada ya kukamatwa ng'ambo na kurudishwa Nigeria.

Kujitenga kwa maeneo ni mada kuu nchini Nigeria, hasa kusini-mashariki ambapo kutangazwa kwa uhuru na Jamhuri ya Biafra kulisababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miezi 30 kati ya mwaka wa 1967 na 1970. Mzozo huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja, hasa kutokana na njaa na magonjwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.