Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Senegal na Guinea-Bissau zaimarisha ushirikiano wao wa kijeshi

Mkuu wa Majeshi ya Senegal, Jenerali Cheick Wade, alifanya ziara nchini Guinea-Bissau Ijumaa Agosti 19, ikiwa ni ziara ya kwanza tangu kutumwa kwa vikosi vya nchi yake ndani ya mfumo wa Ujumbe wa kuunga mkono utulivu wa Guinea- Bissau (MASG). Ziara hii pia ni sehemu ya uimarishaji wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Dakar na Bissau.

Huko Casamance, nchini Senegal, jeshi linahakikisha kuwa hali inadhibitiwa kwenye mpaka na Guinea Bissau baada ya wiki mbili za operesheni dhidi ya ngome za wapiganaji wa MFDC (Februari 9, 2021).
Huko Casamance, nchini Senegal, jeshi linahakikisha kuwa hali inadhibitiwa kwenye mpaka na Guinea Bissau baada ya wiki mbili za operesheni dhidi ya ngome za wapiganaji wa MFDC (Februari 9, 2021). © Charlotte Idrac
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya saa 24 ilimwezesha mkuu wa jeshi la Senegal, Jenerali Cheikh Wade, kukutana na kamandi ya vikosi vya Senegal vilivyowekwa nchini Guinea-Bissau tangu mwezi Juni mwaka jana kama sehemu ya ujumbe wa kusaidia kuleta utulivu nchini Guinea-Bissau (MASG) .

Doria ya pamoja

Katika nyanja ya nchi mbili, mikataba kadhaa kwa sasa inasimamia ushirikiano wa kijeshi, ambayo ni kubadilishana habari hasa, doria ya pamoja kwenye mpaka wa pamoja na mafunzo ya maafisa wakuu wa Guinea-Bissau nchini Senegal. Hata hivyo, mkuu wa jeshi la Guinea-Bissau, Jenerali Biagué Na Ntan, anataka uhusiano huu kuimarishwa.

Guinea-Bissau na Senegal zinashiriki kilomita 338 za mpaka wa pamoja, ambapo uasi umekuwa ukiendelea kwa miaka arobaini. Suala hili halijatolewa hadharani. Hata hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya waangalizi, inasalia kuwa kiini cha mkutano kati ya wajumbe hao wawili.

Silaha kukusanywa

Kama sehemu ya makubaliano yaliyotiwa saini Agosti 4 kati ya kundi la wanaotaka kujitenga kwa eneo la Casamance na serikali ya Senegal, Guinea-Bissau ilmepewa jukumu, kama mdhamini wa kusimamia ugawaji na ukusanyaji wa silaha za waasi, kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.