Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- TIGRAY-MAREKANI

Marekani inataka kurejelewa kwa mazungumzo ya upatikanaji wa amani Ethiopia.

Mjumbe maalum wa Marekani kwenye pembe ya Afrika ametaka kurejelewa kwa mazugumzo ya upatikanaji wa amani nchini Ethiopia pamoja na kuondolewa vikwazo dhidi ya usafirishaji wa misaada katika baadhi ya sehemu nchini humo.

Wapiganaji wa TPLF nchini Ethiopia Juni 2021.
Wapiganaji wa TPLF nchini Ethiopia Juni 2021. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Mike Hammer, ambaye yuko jijini Addis Ababa, amefanya mazungumzo na naibu wa waziri mkuu na waziri wa mambo ya kigeni Demeke Mekonnen.

Ubalozi wa Marekani kupitia ukurasa wake wa twita, umesema kuwa wawili hao wamejadiliana kuhusu usafirishaji wa bidhaa za misaada, ulinzi wa haki za binadamu pamoja na upatikanaji wa suluhu la kisiasa kumaliza machafuko nchini humo.

Serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed na wapiganji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) wameonyesha nia ya kufanya mazungumzo ya amani kumaliza mapigano yalioaanza Novemba 2020.

Licha ya hakikisho la  pande hizo mbili la kutaka kufanyika kwa majadiliano, swala la ni nani atakayeongoza mazungumzo hayo limeibua utata.

Abiy kwa upande wake anataka umoja wa Afrika wenye makao yake jijini Addis Ababa, kuwa mpatanishaji wakati ambapo TPLF nayo ikitaka nchi jirani ya kenya kuwa mpatanishaji.

Mshauri wa Abiy kuhusu masuala ya usalama wa taifa Redwan Hussein katika ukurasa wake wa twita,amesema kuwa serikali iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote popote pale

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.