Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Uhuru Kenyatta: Ruto anasema uwongo kuhusu miradi ya serikali

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kwa mara nyingine ameonesha kugadhabishwa na kile anachosema uongo unaosemwa na naibu wake William Ruto, kuhusu miradi ya Serikali na hasa suala nyeti la Bandari ya Mombasa.

Rais wa Kenya -Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya -Uhuru Kenyatta REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati akiwa mjini Naivasha, Kenyatta amesema kuwa kinyume na anavyosema naibu wake mradi huo hautaathiri namna ambavyo shughuli za bandari ya Mombasa zitakavyokuwa zinaendelezwa.

Kwa majuma kadhaa muungano wa kisiasa unaoongozwa na naibu wa rais Ruto, umekuwa ukidai kuwa rais Kenyatta amehujumu bandari ya Mombasa, madai ambayo Kenyatta, ameyakanusha vikali.

“Zile kontena zitakuwa zikitoka hapa kwani zitakuwa zinapitia wapi? Si hiyo ni kazi tumepatia wenzetu wa Mombasa, Watu wa Mombasa wamefaidika, watu wa Naivasha wamefaidika na kiongozi anasimama akidaganaya mchana mchana. Hakuna mtu amefutwa Mombasa ati kwa sababu ya hii kazi, kwanza watakapoanza kulingana na vile wametuambia nchi ya kenya kila mwaka itakuwa ikizalisha zaidi ya nusu bilioni dolla sio shillingi dolla” amesema rais Kenyatta.

Tangu rais Kenyatta afikie maridhiano na aliyekuwa kinara wa upinzani Raila Odinga, uhusiano Wake na aliyekuwa mwandani Wake William Ruto, ulizorota kila mmoja akimtuhumu mwingine kwa usaliti.

Ruto aidha amekuwa akimtuhumu rais Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kwa kuchangia pakubwa katika mgogoro wa kichumi unaolikabili taifa hilo la Afrika mashariki. Ruto na mrengo wake wanahisi kuwa mapatano kati ya wawili hao yamesababisha viwango vya ufisadi kuongezeka nchini kenya.

Raila Odinga anaungwa mkono na rais Kenyatta kumrithi baada ya uchaguzi mkuu wa agosti 9, Kenyatta akisema kuwa alichukua hatua hiyo kutokana hiyo kwa sababu anaamini kuwa Odinga ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mpizani wake kisiasa ndiye mtu anayefaa kumrithi na kuendeleza sera zake.

Rigathi Gachagua,mgombea mwenza wa William Ruto katika mdahalo wa televisheni wa juma lililopita alisema asasi muhimu za serikali kama vile idara ya uchunguzi DCI zimetekwa na serikali swala alilosema limechangia pakubwa katika matatizo yanyolikumba taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.