Pata taarifa kuu
UFARANSA- AFRIKA MAGHARIBI

Macron yuko nchini Benin kwa mazungumzo kuhusu usambazaji chakula na usalama

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amefanya mazungumzo na rais wa Benin Patrice Talon katika ziara yake ya siku ya pili kwenye mataifa ya Afrika magharibi.

Rais wa Benin Patrice Talon na  Emmanuel Macron wa Ufaransa
Rais wa Benin Patrice Talon na Emmanuel Macron wa Ufaransa © AFP/Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya rais Macron imekuja wakati huu ambapo idadi kubwa ya wabunge kutoka vyama vya upinzani nchini Ufaransa wakionya kuhusu kuongezeka kwa visa vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Benin

Rais Macron anatarajiwa kukamilisha ziara yake ya kikazi ya siku nne nchini Guinea-Bissau siku ya alhamis, hii ikiwa ziara yake ya kwanza barani Afrika katika kipindi cha muhula wake wa pili afisini.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona kuwa zaira ya Macron katika ukanda wa Afrika magharibi inalenga kujenga upya uhusiano wa kidiplomasia ulioyumba   na  mataifa yaliokuwa koloni ya Ufaransa.

Agenda kubwa katika kikao cha leo Jumatano imekuwa kuhusu usambazaji wa chakula, mazungumzo yanyokuja wakati huu ambapo bara Afrika likihofia kumbwa na uhaba wa nafaka kutokana na mzozo kati ya Urusi na Ukraine.

Ziara hii pia imekuja baada ya wabunge 75 wa upinzani kumuandikia rais huyo barua wakilalamikia ongezeko la wafungwa wa kisiasa nchini Benin utawala wa rais Talon ukitajwa kuwalenga wapinzani.

Swala la usalama limepewa kipau mbele katika ziara ya Macron katika mataifa hayo ya Afrika Magharibi haswa wakati huu ambapo Ufaransa inajiaanda kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali. Hatua inayokuja wakati huu pia ukanda huo ukiendelea kabiliwa na tishio la ongezeko ya makundi yenye silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.