Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Azimio la umoja kufanya mkutano wa mwisho agosti 6 kasarani

Muungano wa siasa wa Azimio la Umoja One Kenya utaandaa mkutano wake wa mwisho kuelekea uchaguzi mkuu wa agosti 9 katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Kasarani jijini Nairobi tarehe 6 ya mwezi ujao.

Mkutano wa kisiasa wa Azimio la umoja -One Kenya  Juni 2 2022 jijini Nairobi
Mkutano wa kisiasa wa Azimio la umoja -One Kenya Juni 2 2022 jijini Nairobi © skmusyoka
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliopita katibu mkuu wa muungano huo Junet Mohammed alikuwa ametangaza kuwa chama hicho cha kisiasa kinachoongozwa na mgombea urais Raila Odinga kingefanya mkutano wake wa kampeni wa mwisho katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Kabla ya mkutano huo, kundi la Azimio limetangaza kuwa litafanya kampeni za mwisho kuelekea mkutano huo mkubwa katika maeneo ya Nakuru, Machakos, Suswa na  Eldoret-eneo linadhaniwa kuwa ngome ya kisiasa ya naibu rais William Ruto.

Hatua hii inakuja baada ya mvutano kati ya Azimio chake Odinga na Kenya Kwanza chake Ruto kuhusu uwanja wa Nyayo kabla ya wizara ya mamlaka inayosimamia viwanja kudhibitisha kuwa uwanja huo ulikuwa umechukuliwa kwa ajili ya mkutano wa maombi.

Mrengo wa Kenya Kwanza nao umeendelea kusisitiza kuwa utaandaa mkutano wao wa mwisho katika uwanja huo wa Nyayo ukisema tayari ulikuwa umelipia ada ya shillingi milioni 1.5 pesa ya kenya kwa mamlaka inayosimamia viwanja vya michezo nchini humo.

Mamlaka hiyo imekana madai kuwa ilikuwa imetoa ruhusu kwa chama cha UDA chake Ruto kutumia uwanja huo kati ya tarehe 5 na 6 mwezi agosti.

Magombea wawili wakuu wa urais wanatarajiwa kuaandaa mikutano yao ya kumaliza kampeni kuelekea uchaguzi wa agosti 9 jijini Nairobi.

Kampeni rasimi ziliaanza kufanyika nchini kenya Mei 30 na zinatarajiwa kumalizika saa 48 kabla ya siku ya  uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.