Pata taarifa kuu
UFRANSA-AFRIKA

Rais Macron ameanza ziara ya siku 3 kwa mataifa ya Afrika Magharibi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameanza ziara ya siku tatu kwa mataifa ya Afrika magharibi ziara ya kwanza katika muhula wake wa pili akitaka kurejesha uhusiano mwema na mataifa yaliokuwa koloni yake katika ukanda wa Afrika.

Rais Emmanuel Macron anazuru Afrika magharibi.
Rais Emmanuel Macron anazuru Afrika magharibi. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Ziara yake rais Macron imeaanzia nchini Cameroon akitarajiwa pia kuzuru Benini kabla ya kumalizia ziara yake nchini Guinea-Bissau.

Akiwa nchini Cameroon rais Macron atakutana na mwenyeji wake Paul Biya, 89, ambaye ametawala taifa hilo linalokumbwa na chanagmoto ya kiusalama kwa miaka 40.

Macron anatarajiwa kuangazia pakubwa swala la upatikanaji wa chakula kwa mataifa ya Afrika haswa wakati huu ambapo bara hilo linahofia kuwa huenda likakumbwa na uhaba wa chakula kutokana na uvamizi wa Urusi kwa taifa huru la Ukraine.

Licha ya hilo, swala la usalama linatarajiwa kujadiliwa pakubwa katika zira hiyo haswa wakati huu ambapo Ufaransa inajiaanda kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali mwaka huu.

Hatua ya Ufaransa kuwandoa wanajeshi wake nchini Mali ikija wakati ambapo mataifa sehemu kubwa ya mataifa ya  Afrika magharibi yanapokabiliwa na tishio la makundi ya wapiganaji wa kiisilamu.

Rais Macron ameahidi kuleta uhusiano mpya kati ya Ufaransa na mataifa ya Afrika haswa baada yake kuchaguliwa kuhudumu kwa awamu ya pili.

Wachambuzi wa maswala ya kisiasa nao wanahisi kuwa ziara ya Macron kwa mataifa hayo huenda pia ikawa ni njia moja ya kujaribu kabiliana na kile ambacho kimetajwa kuwa tishio kutoka kwa  mataifa kama Uturuki, China na Urusi kuaanza kuingia katika ngome ambazo zimekuwa zitawaliwa pakubwa na taifa lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.