Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Mdahalo wa wagombea urais kuendelea licha ya Odinga kutishia kujiondoa

Mdahalo wa wagombea urais ulioratibiwa kufanyika Jumanne ya Julai 26 utandelea kama ulivyopangwa licha ya tishio la mgombea urais kupitia chama cha Azimio la umoja one kenya, Raila Odinga kutoshiriki.

Wagombea wawili wakuu wa urais nchini Kenya ,Raila Odinga na Naibu rais William Ruto
Wagombea wawili wakuu wa urais nchini Kenya ,Raila Odinga na Naibu rais William Ruto © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa kamati inayopanga mdahalo huo Clifford Machoka, amesistiza kuwa shughuli hiyo itafanyika kama ilivyoratibiwa kuaanza Jumanne saa kumi jioni hadi saa nne usiku za Afrika mashariki.

Kwa mujibu wa Machoka, kamati yake tayari imewafahamisha wagombea watakaoshirki mdahalo huo baadhi ya maswala yatakayojadiliwa na wasimamizi wa shughuli watahakikisha yamezungumziwa.

Aidha wasimamizi wa mdahalo huo watachagua maswali ya kuwauliza wagombea wakati wa shughuli hiyo ya hapo kesho jioni.

Kulingana na sheria na mwongozo wa mdahalo huo,wasimamizi hawaruhusiwi kukutana na wagombea au wanachama wa mirengo yao ya kampeni hadi pale ambapo shughuli hiyo itakuwa imemalizika.

Tangazo la kamati hiyo limekuja ikiwa imepita siku moja baada ya timu inayosimamia kampeni zake Odinga kutangaza kuwa kinara wao hatashirki zoezi hilo.

Katika taarifa yake Odinga alisema kuwa swala la kushiriki mdahalo na naibu wa rais William Ruto halikuwa wazo zuri.

Tangazo la Odinga kutishia kutoshiriki shughuli hiyo likija baada ya mgombea mwengine wa urais kupitia chama cha Roots George Wajackoyah kutaka mdahalo huo kushirikisha wagombea wote kwa wakati mmoja naye pia akitishia kutoshiriki iwapo hilo halitazingatiwa.

Chama cha Roots kimesisitiza kuwa kitashiriki iwapo mgombea wake atajumuishwa katika mdahalo pamoja na Odinga na Ruto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.