Pata taarifa kuu
Mali - Diplomasia

Togo : Yaanza upatanishi kuhusu mzozo wa Mali na Ivory Coast

Waziri wa mambo ya nje wa Togo, Robert Dussey amefanya mazungumzo na maafisa wa serikali ya Ivory Caost kuhusiana na kukamatwa kwa wanajeshi wake 49 nchini Mali, mapema mwezi huu.

Robert Dussey, waziri wa mambo ya nje wa Togo
Robert Dussey, waziri wa mambo ya nje wa Togo AFP/Georges Gobet
Matangazo ya kibiashara

Waziri Dussey amesema rais wa Ivory Coast Alassane  Ouattar, na kiongozi wa kijeshi nchini Mali, Assimi Goita, wameonesha nia ya kuzuia mvutano kuendelea  kati ya mataifa hayo mawili.

Mkutano wa Dussey unajiri baada ya Mali kupendekeza Togo kuwa mpatanishi kati yake na Ivory Coast.

49 hao walimatwa mara  baada ya kutua jijini Bamoka, serikali ya Mali, ikiwatuhumu kuwa mamluki waliolenga kuyumbisha serikali.

Hata hivyo Ivory Coast inasisitiza kuwa wanajeshi hao walikuwa miongoni mwa ujumbe wa Umoja wa mataifa unaoshika doria nchini Mali, Minusma, chini ya makubaliano baina ya mataifa hayo mawili.

Utawala wa kijeshi nchini Mali, unasema wizara ya mambo ya nje ya haikuwa na taarifa kuhusiana na ujio wa wanajeshi hao nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.