Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: EU kusambaza waangalizi 180 wakati wa uchaguzi mkuu wa agosti 9

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya raia nchini Kenya kupiga kura katika uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu, tayari mashirika ya kiraia ya ndani na yale ya kimataifa yameanza kufuatilia mchakato wa uchaguzi huo.

Wagombea wakuu wa urais nchini kenya Raila Odinga na William Ruto.
Wagombea wakuu wa urais nchini kenya Raila Odinga na William Ruto. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikumbukwe kuwa mwaka 2017 mahakama ya juu ilifuta uchaguzi huo kwa dosari zilizojitokeza, na kusambazwa kwa waangalizi kama ilivyo kwa umoja wa Ulaya, ni kujaribu kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani.

Tayari umoja wa ulaya umetangaza kutuma waangalizi 180, ambapo 48 tayari wamewasili, huku gharama za waangalizi hao zikitajwa kufikia euro milioni 8.

Ivan Shtefanek kiongozi wa ujumbe wawaangalizi wa umoja wa Ulaya amezungumzia hatua ambazo wamezipiga kwa sasa.

“Tumeanza kufuatilia kampeni, na tutaendelea kufuatilia hadi baada ya uchaguzi. Siku ya uchaguzi tutaangalia ufunguzi wa vituo, upigaji kura pamoja na utangazaji matokeo. Tunaamini uchaguzi utakuwa huru na kuaminika.” amesema Ivan Shtefanek

Hata hivyo tayari waangalizi hawa wameonesha masuala kadhaa ambayo ni lazima tume ya uchaguzi iyaangalie kwa umakini. Beata Martin Ruzo-Milo-Vich, naibu kiongozi wa waangalizi kutoka umoja wa Ulaya kwa upande wake naye ameelezea mipango yao kuelekea uchaguzi huo.

 “Tutafuatilia hatua zote za uchaguzi ambazo raia wakenya wanawasiwasi nazo, inaanzia katika kuheshimu sheria, sajili ya wapigakura n ahata kampeni. Pia tutaangalia mchango wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, pamoja na matumizi ya teknolojia kwaajili ya uchaguzi au mchango wa wanawake na makundi mengine.” ameelezaMartin Ruzo-Milo-Vich

Aidha umoja wa Ulaya umepongeza juhudi za shirika la kiraia la nchini Kenya ELOG ambalo litatuma waangalizi elfu 5, sawa na umoja wa Afrika na Igad, ambao nao wametangaza kutuma waangalizi wao.

Hatua hii inakuja wakati huu ambapo wagombea wakuu wawili ambao ni waziri mkuu wa zamani Raila Odinga anayegombea kupitia chama cha Azimio la umoja one kenya na naibu wa rais William Ruto wa UDA wakiendelea kushtumia kwa madai ya njama ya wizi wa kura wakati wa uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki IEBC, imewahakikishia wapiga kura nchini humo uchaguzi wa huru na wa haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.