Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya: Kinyang'anyiro ni kati ya Odinga na Ruto ,kura ya maoni

Kura mpya ya maoni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi ujao nchini Kenya, imeonesha mchuano mkali utakuwa baina ya wagombea wawili wanaopewa nafasi kwenye uchaguzi huo, licha yakuwa wagombea wengine wawili wameendelea kujizolea umaarufu.

Mabango ya wagombea wakuu wa urais nchini kenya katika uchaguzi wa agosti 9 Raila Odinga na William Ruto.
Mabango ya wagombea wakuu wa urais nchini kenya katika uchaguzi wa agosti 9 Raila Odinga na William Ruto. © RFI/Robert Minangoy
Matangazo ya kibiashara

Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya Infotraka kati ya tarehe mbili na saba mwezi huu,umeonesha wagombea wawili wakuu Raila Odinga na William Ruto wameachana tu na asilimia sita .

Serikali kwa upande wake ,ikikiri kuongezeka joto la kisiasa kuelekea kura hizo,imeendelea kuahidi kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa njia salama.

Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi  amewataka wanasiasa kuachana na matukio au matamshi yanayoweza kutatiza usalama wa uchaguzi.

Uongozi wa kampeni wa Azimio ukiendelea kuitaka  tume ya uchaguzi  na mipaka kumaliza mgogoro ndani yake ambayo yanaweza kusababisha vurugu wakati wa kura hizo.

Wafula Chebukati mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi kwenye taifa hilo la Afrika mashariki, akihojiwa na waandishi wa habari amewahakikishia wakenya kuwa tume yake iko tayari kwa uchaguzi wa agosti tisa, akitupilia mabali madai ya kuwepo kwa mgawanyiko kati ya maofisa wake.

Mwenyekiti huyo aidha amesisitiza uhuru wa tume yake akieleza kuwa haitaegemea upande wote wote wa kisiasa na iko tayari kutangaza matokeo ya uwazi, uhuru na haki.

Joto la kisiasa nchini Kenya limepanda kuelekea uchaguzi wa tarehe tisa mwezi ujao, huku wito wa Amani ukitolewa kwa wanasiasa na wananchi.

Naibu wa rais William Ruto , na mrengo wake amekuwa akiituhumu mpizani mwake mkubwa Raila Odinga kwa kutumia mali ya serikali kufanya kampeni , Odinga naye akimtuhumu Ruto kwa kufeli kuwashugulikia wakenya wakati akiwa katika uwongozi kwa kipindi cha miaka 10.

Raila Odinga wa Azimio la umoja , Willima Ruto wa kenye kwanza, George Wajackoyah wa chama cha roots party na David Mwaure wa chama cha agano ndiyo wagombea wanne walioidhinishwa na Iebc kuwania katika uchaguzi huo ila upinzani mkubwa ni kati ya Odinga waziri mkuu wa zamani na Ruto naibu wa rais wa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.