Pata taarifa kuu
MOROCCO -USALAMA

Morocco: Wahamiaji haramu 257 wamezuiwa kuelekea bara Europa.

Jeshi la wanamaji la Morocco limeripoti kuwa katika kipindi cha siku nne limewazuia wahamiaji haramu zaidi ya 257 waliokuwa na ni ya kuvuka kwenda bara Europa.

Wahamiaji haramu baada ya kuokolewa katika bandari ya  Malaga, kusini mwa Hispania.
Wahamiaji haramu baada ya kuokolewa katika bandari ya Malaga, kusini mwa Hispania. © Reuters/Jon Nazca/(File photo/2019)
Matangazo ya kibiashara

Hatua inayokuja zikiwa zimepita wiki mbili baada ya kutokea mkanyagano katika eneo la mpaka ambapo watu 23 walifariki.

Wengi wa wahamiaji hayo wamesemekana kutokea katika mataifa ya Afrika, ambapo pia walikuwemo raia wawili wa Afghanistan na Yemen.Watoto pia wakisemekana kuwemo kwenye chombo walichokuwa wanasafiria.

Mwezi Jana, karibia wahamiaji 23 walifariki baada ya kukanyagana walipokuwa wanajaribu kupanda kuta za mpaka wa kuingia nchini Hispania.

Mashirika ya kiraia katika ripoti yake nayo yanasema kuwa karibia watu 37 walifariki wakati wa tukio hilo, idadi ambayo ni kubwa kuliko ile iliyotolewa na mamlaka husika.

Mamlaka nchini Morocco zilieleza kuwa waliofariki walikuwa miongoni mwa karibia watu elfu mbili wengi wao wakiwa raia wa Sudan waliojaribu kuvuka mpaka huo kwa nguvu.

Wahamiaji ambao kwa mara mingi wanakimbia mapigano, usalama wa chakula katika mataifa yao wamekuwa wakijaribu kuingia nchini Hispania kwa kutumia maboti.

Zaidi ya wahamiaji 40,000, wengi wao wakitokea nchini Morocco, waliripotiwa kuwasili nchini Hispania mwaka wa 2021 wakitumia usafiri wa maji kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya usalama wa ndani.

Katika kipindi cha miezi mitano katika  mwaka huu wa 2022, idadi ya wahamiaji iliongezeka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka wa 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.