Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- USALAMA.

Uhuru Kenyatta aongoze mazungumzo na Addis Ababa: Wapiganaji wa Tigray.

Wapiganaji waasi wa kundi la Tigray, ambao kwa muda sasa wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Ethiopia tangu mwezi Novemba 2020, wanasema kuwa wako tayari kutaja kikosi cha watu wataongoza mazungumzo na Addis Ababa,imesema taarifa ya mwakilishi wa mambo ya nje wa  Tigray representative Kindeya Gebrehiwot.

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed akizungumza katika bunge la nchi hiyo mwaka wa 2020. .
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed akizungumza katika bunge la nchi hiyo mwaka wa 2020. . © AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Juni 4, waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed aliashiria uwezekano wa serikali yake kufanya mazungumzo na wapiganji wa wa kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF), kundi la waasi ambalo lilitawala  siasa za Ethiopia kwa karibia miongo mitatu.

Licha ya kauli yake waziri mkuu Abiy Ahmed, kundi la TPLF limendelea kusistiza kuwa liko tayari kushiriki mazunguzmo na serikali yake Abiy Ahamed iwapo kikao hicho kitafanyika chini ya uwongozi wa uhuru Kenyatta, rais wa kenya.

TPLF aidha linataka taifa la Marekani, waakilishi wa umoja wa ulaya na wale wa umoja wa mataifa pamoja na umoja wa Afrika kushiriki katika mazungumzo yao na serikali ya Ethiopia.

Tayari serikali ya Ethiopia imetaja kundi la wapatanishi saba wakiongozwa na naibu waziri mkuu Demeke Mekonnen kufanya mazungumzo la TPLF kama njia moja ya kumaliza mapigano ya miezi 18 kaskazini mwa Ethiopia.

Awali mazungumzo hayo yalikuwa yameratibiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu japokuwa hayakufanyika.Hadi sasa bado haijabainika ni wapi mazunguzmo hayo yatafanyika ila TPLF inasema kuwa swala hilo bado linaendelea kujadiliwa.

Maofisa wa TPLF, wameishutumu serikali ya Ethiopia kwa madai ya kutonyesha kujitolea kwake kufanikisha mazungumzo ya kuleta amani katika jimbo la Tigray.

Mjumbe maalumu wa umoja wa Afrika (AU),rais wa zamani wa Nigeria  Olusegun Obasanjo, katika siku za hivi karibuni amekuwa akifanya vikao vya kila mara na TPLF na viongozi wa serikali ya Ethiopia kama njia moja ya kuleta pande husika kwa meza ya mazungumzo.

Machafuko jimboni Tigray yalizuka Novemba 2020 na hadi sasa yamegarimu maisha ya maelfu ya watu ambapo pia yamebabisha mzozo wa kiraia katika eneo hilo asilimia 90 ya raia wa Tigray wakikumbwa na baa la njaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.