Pata taarifa kuu
Somalia - Chakula

UN: Somalia yazama kwa baa la njaa

Umoja wa mataifa umeonya kuwa mikowa nane kati ya 18, nchini Somalia ipo kwenye hatari ya kushuhudia baa la njaa, kufikia mwezi Septemba, kutokana na kipindi kirefu cha cha ukame na vita vinayoendelea nchini Ukraine.

Chakula cha msaada
Chakula cha msaada AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Stéphane Dujarric, amesema licha ya kwamba zaidi ya watu millioni 4 wamepokea msaada tangu mwezi Junuari, Umoja huo bado unahitaji pesa zaidi ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji na njaa.

Aidha tayari watoto 200, wamefariki tangu mwezi Januari,  nchini Somalia kutokana na utapilia mlo, huku idadi ya watu wanaoshuhudia ukosefu wa chakula ikiongezeka kutoka millioni 4.5 hadi Millioni 7.

Kauli hii inajiri wakati huu shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, likisema asimilia 10 ya raia duniani wameathirika na wanakabiliwa na baa la njaa.

Mataifa ya pembe ya Africa na eneo la Sahel yakiwa ndiyo yalioathirika zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.