Pata taarifa kuu
Kenya- Ethiopia - Usalama

Kenya : Yawakabidhi raia wanne wa China kwa mamlaka ya Ethiopia

Serikali ya Kenya imewakabidhi raia wanne wa China kwa serikali ya Ethiopia, kwa  kutuhumiwa za mauwaji ya mwenzao nchini Ethiopia, na baadaye  kukimbilia nchini Kenya.

Polisi wakiendesha oparesheni ya kuwasaka wahalifu
Polisi wakiendesha oparesheni ya kuwasaka wahalifu ABDULMONAM EASSA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanne hao wanatuhumiwa kumuua mwenzao aliyetambuliwa kama Fu Hui, katika mkahawa mmoja wa kichina jijini Addis Ababa, kabla ya kutorokea nchini Kenya.

Mkuu wa idara ya polisi nchini Ethiopia, Tsegaye Haile, amesema washukiwa  Huang Zhipeng, Liv Jie, Wang Ming na Chao Fu Xiuzaong, walikamatwa kutokana na opeseheni ya pamoja ya mamlaka za Kenya na Ethiopia.

Kisa hiki kinajiri baada ya mwezi Februari, mwaka huu Kenya na Ethiopia kukubaliana kushirikiana katika vita vya pamoja vya kupamba na ugaidi maeneo ya mipakani, lengo likiwa kupambana na kundi la kigaidi la Somalia la Al-Shabaab na lile la Ethiopia la OLF-Shene.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.