Pata taarifa kuu

Mali yaanza kuwaondoa wanajeshi wake kutoka G5 Sahel

Bamako ilitangaza mnamo Mei 15 kujiondoa kwake kutoka kwa kikosi cha G5 Sahel, baada ya kubaini kuwa haikukubaliwa kuongoza jumuiya hiyo, wakati ilikuwa ni zamu yake.

G5 Sahel hatarini, baada ya kujiondoa kwa Mali.
G5 Sahel hatarini, baada ya kujiondoa kwa Mali. © AFP-Sebastien Rieussec
Matangazo ya kibiashara

Kundi la G5 ni muungano wa kisiasa na kijeshi unaoleta pamoja Mali, Niger, Burkina Faso, Mauritania na Chad, na moja wapo ya malengo yake kuu ni mapambano dhidi ya ugaidi.

Chad hata hivyo ilikuwa imejaribu kuokoa G5, ikiomba Mali kufikiria upya uamuzi wake na kufanya kazi kutafuta njia ya kutoka katika mgogoro huo. Lakini mamlaka ya Mali haijabadili msimamo wake: ilitoa maelekezo ya kuwatenganisha wanajeshi wa Mali walioingizwa katika kikosi cha pamoja cha G5 katika siku chache zijazo.

Mkuu wa Majeshi ya Mali ndiye ambaye alitoa agizo hilo mnamo Jumanne, Juni 14. Katika hati iliyoainishwa, ambayo imevuja kwa, Jenerali Oumar Diarra amesiisha ushirikiano wa askari wa Mali waliopewa kazi ya kamandi ya G5 huko Bamako, ukanda wa magharibi wa Nema nchini Mauritania, na ukanda wa katikati huko Niamey nchini Niger. Kwa jumla, karibu askari 1,400, kati ya 5,000 wanaounda kikosi cha pamoja cha G5 wameondolewa katika kikosi hiki.

Mipango pia imefanywa ya kuwarejesha nyumbani wanajeshi wa Mali walioko katika nchi jirani. Kwa wale walio mjini Bamako, watatumwa kwa idara zao za awali kuanzia Julai 1, baada ya wiki mbili.

Chad ilikuwa imetuma mjumbe kwa haraka Bamako, ili kujaribu kumshawishi rais wa mpito wa Mali, Kanali Assimi Goïta, kutafakari upya uamuzi wake. Mashauriano pia yalikuwa yamezinduliwa na wanachama wengine wa G5 kujaribu kujibu wasiwasi ya Mali na kuokoa jumuiya hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.