Pata taarifa kuu

Ufaransa yamkamata afisa mwandamizi wa IS

Ufaransa inamshikilia Oumeya Ould Albakaye, afisa mwandamizi wa kundi la Islamic State katika ukanda wa Grand Sahara.

Wanajeshi wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane waendelea kuwakamata viongozi wa kundila Islamic State katikaukanda a Grand Sahara.
Wanajeshi wa Ufaransa kutoka kikosi cha Barkhane waendelea kuwakamata viongozi wa kundila Islamic State katikaukanda a Grand Sahara. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo mwandaizi wa kundila IS amekamatwa nchini mali kwenye eneo la mpaka na wanajeshi wa Ufaransa, wakati ambapo wanaingia katika awamu ya kuiondoka nchini humo, makao makuu ya jeshi la Ufaransa yameliambia shirika la habari la AFP Jumatano hii Juni 15, 2022.

"Usiku wa tarehe 11 kuamkia tarehe 12 Juni, operesheni ya kikosi cha jeshi la Ufaransa cha Barkhane iliwezesha kumkamata Oumeya Ould Albakaye, afisa mwandamizi wa kundi la Islamic State", chanzo hiki kimebaini.

Albakaye alikuwa kiongozi wa kundi hilikatika eneola Gourma, nchini Mali, na katika eneo la Oudalan kaskazini wa Burkina Faso, kwa mujibu wa makao makuu ya jeshi la Ufaransa.

"Alifanya mashambulizi mengi dhidi ya vikosi vya kigeni nchini Mali, likiwemo lile lililotokea katika mkoa wa Gao Anahusika na mashambulizi na mauaji dhidi ya raia wengi wa Mali na Burkina Faso", chanzohiki kimeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.