Pata taarifa kuu

Mali: Jeshi laweka makataa ya miaka miwili kabla ya raia kurejea madarakani

Agizo hilo lililotiwa saini na mkuu wa utawala wa kijeshi, Kanali Assimi Goïta, ilisomwa Jumatatu jioni kwenye televisheni ya serikali ya Mali. Hatua moja mbele kwa sababu mwanzoni mwa mwaka, jeshi lilipanga kuiongoza Mali kwa hadi miaka mitano na ECOWAS ilipitisha vikwazo vikali dhidi ya Bamako.

Kanali Assimi Goïta kiongozi wa CNSP, kundi la maafisa waliofanya mapinduzi nchini Mali.
Kanali Assimi Goïta kiongozi wa CNSP, kundi la maafisa waliofanya mapinduzi nchini Mali. MALIK KONATE / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Muda wa kipindi cha mpito umewekwa kuwa miezi 24, (kutoka) Machi 26, 2022", kulingana na agizo lililotiwa saini na kiongozi wa utawala wa kijeshi Assimi Goïta na kusomwa kwenye runinga ya serikali Jumatatu jioni. Kwa hiyo jeshi litashikilia madaraka hadi mwezi Machi 2024 kabla ya kurejesha mamlaka kwa raia.

Tangazo hilo lilimewashangaza wengi nchini Mali. Hata mawaziri wa serikali wamesema faraghani wamesikia habari kwenye runinga kama raia wengine. Kwa upand wa kambi ya Kanali Assimi Goïta, wametetea sheria hiyo: "Lazima twende haraka ili tusipoteze muda", mmoja wa washauri wake ameiambia RFI. "Muda wa kipindi cha mpito wa miezi 24, tayari ni msingi wa majadiliano na ECOWAS, na kile ambacho jumuiya hiyo inatarajia kutoka kwetu sasa ni maelezo juu ya ratiba ya shughuli za kuelekea uchaguzi," kimeongeza chanzo hicho.

Kwa upande wa ECOWAS, afisa mmoja anasema "ameshangazwa" na tangazo hili. Wazo lililoamuliwa baada ya mkutano ni kwamba mpatanishi katika mzozo wa Mali Goodluck Jonathan akutane na wadau wote na kupendekeza mpango wa kumaliza mgogoro huo katika mkutano ujao uliopangwa kufanyika mapema Julai mjini Accra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.