Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais Nigeria: Chama tawala chashindwa kumpata mgombea wake

Wiki moja baada ya upinzani, ni zamu ya chama tawala kuchagua mgombea katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2023. Wanasiasa 23 wa walio wengi wanatarajiwa kupata uungwaji mkono kutoka wajumbe wa chama tawalacha Congress of Progressives, APC.

Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi uliopita wa rais nchini Nigeria.
Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi uliopita wa rais nchini Nigeria. AFP PHOTO/Tom Saater
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa wiki hii iliyopita, Rais Muhammadu Buhari aliomba chama chake kukubaliana juu ya mgombea mmoja "kabla ya Jumatatu", lakini ni vigumu kufikia makubaliano.

Mazungumzo yalianza kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkataba wa APC siku ya Jumatatu. Rais Muhammadu Buhari, msuluhishi mkuu wa katika uchaguzi huu wa mchujo, amezidisha mashauriano wikendi nzima. Hasa, aliwaitisha wagombea wote kuja kwenye makazi yake huko Aso Rock Jumamosi jioni.

Mgombea "wa mmoja pekee".

Mkuu wa nchi aliwataka kutafuta mwafaka na kuteua mgombea "wa kipekee" siku ya Jumatatu. Hakuna kinachojulikana, hata hivyo, kuhusiana na chaguo la Rais Buhari mwenyewe, ambaye hata hivyo anaweza kuwa na uzito mkubwa katika uchaguzi huo.

Tukio lingine muhimu wikendi hii: magavana kumi na mmoja kutoka kaskazini mwa Nigeria, ambao wengi wao ni Waislamu, wamejitokeza kuunga mkono mgombea kutoka kusini mwa nchi hiyo, ambao wengi wao ni Wakristo. Pendekezo ambalo lilikaribishwa na gavana wa zamani wa Lagos, Bola Tinubu, ambaye ni mmoja wa wagombea katika uchaguzi huu wa mchujo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.