Pata taarifa kuu
Ethiopia Siasa

Ethiopia : Jenerali Tefera Mamo akamatwa

Aliyekuwa kamanda vikosi vya Amhara nchini Ethiopia, jenerali Tefera Mamo, anazuiliwa katika jijini la Bahir Dar, baada yake kutoweka kwa mazingira yasiyoeleweka siku ya jumatatu jiji Addis Ababa.

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed © AP
Matangazo ya kibiashara

Mke wa Mamo, Menen Haile, amesema amethibitisha mumewe anazuiliwa katika eneo la Bahir Dar, baada ya kukamatwa kwa tuhuma zisizojulikana siku ya jumatatu.

Jenerali Mamo aligonga vichwa vya habri mwezi wa pili mwaka huu baada ya kuondolewa katika wadhifa wake, na haijafahamika wazi ninini kimechangia kukamatwa kwake.

Kiongozi wa jimbo la Amhara, Yilkal Kefale, kupitia taarifa amesema, kuna baadhi ya washukiwa wanaoshikiliwa na polisi kwa lengo la kuhakikisha Ethiopia ina Amani, na kwamba wale ambao hawana hatia wataachiliwa hivi karibuni.

Mwaka 2009, jenerali Mamo alifungwa jela baada ya kuhusishwa na mpango wa kutaka kuipindua serikali ya waziri mkuu wa zamani, Male Zenawi, ila akachiliwa mwaka 2018, wakati wa mageuzi ya kisiasi nchini Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.