Pata taarifa kuu
Siasa Mali

Mali : Serikali yazuia mapinduzi mengine

Serikali ya kijeshi nchini Mali imesema ilizuia jaribio la mapinduzi ya serikali, jaribio ambalo lilifadhiliwa na mataifa ya magharibi kupitia kwa wanajeshi waatiifu kwa mataifa hayo.

Rais wa  Mali Assimi Goita.
Rais wa Mali Assimi Goita. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa uongozi wa kijeshi nchini Mali, umesema jaribio hilo la mapinduzi lilifanyikaa usiku wa tarehe 11 na 12 mwezi huu.

Bila kutoa maelezo Zaidi serikali ya Mali, imesema  jaribio hilo la kupindua serikali lilikabiliwa kitaalamu na waliohusika wapatao maafisa 10 wa jeshi watakabiliwa kisheria, bila pia kutaja wahusika.

Wanajeshi wa Mali wametekeleza mapinduzi ya serikali mara mbili tangu mwaka 2020, baada ya kumuondoa madarakani rais Ibrahim Keita, utawala wa sasa ukishinikizwa kurejesha utawala wa kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.