Pata taarifa kuu

Somalia: Wabunge wanajianda kupiga kura Jumapili 15 kumchagua rais.

Wabunge nchini Somalia wanajiandaa kupiga kura siku ya Jumapili, kumchagua rais, uchaguzi ambao ulikuwa umepangwa kufanyika mwaka uliopita, lakini ukacheleweshwa kwa sababu za tofauti za kisiasa.

Shugaban kasar Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo
Shugaban kasar Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kufanyika kwa kuchelewa, hatua ya kufanyika kwa uchaguzi huo, imesifiwa na Jumuiya ya Kimataifa, baada ya hofu ya hapo awali kuwa tofauti za kisiasa zingerudisha nyuma hatua za kisiasa zilizopigwa katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Hata hivyo, kwa mara nyingine baada ya miaka hamsini Somalia imeshindwa kuandaa uchaguzi ambao wananchi watapata nafasi ya kumchagua kiongozi wao, na badala yake mamlaka hiyo imetwikwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.

Kwa kipindi hicho chote, wananchi wa Somalia, wameshindwa kupiga kura kwa sababu za kiusalama, vikwazo vya kisheria na changamoto za fedha.

Maseneta 54 na wabunge 275 waliochaguliwa na wajumbe wa koo mbalimbali kutoka majimbo matano ya Somalia, wameachiwa jukumu hilo kumchagua rais mpya.

Uchaguzi huu umewavutia wagombea 39, idadi kubwa katika historia ya nchi hiyo, akiwemo rais wa sasa Mohammed Farmajo na rais wa zamani, Hassan Sheikh Mohamud, miongoni mwa wengine akiwemo mwanamke mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.