Pata taarifa kuu

Nigeria: Zaidi ya watoto milioni 18 hawako shuleni, kulingana na UNICEF

Shirika la kulinda haki za watoto katika umoja wa mataifa UNICEF, linasema kuwa zaidi ya watoto milioni 18.5 nchini Nigeria hawana uwezo wa kupata elimu, nusu ya idadi hiyo wakiwa ni watoto wa kike.

Wanajeshi wa Nigeria wakilinda shule katika eneo Chibok
Wanajeshi wa Nigeria wakilinda shule katika eneo Chibok news.softpedia
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizi za hivi punde za UN, zinaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watoto wasio na uwezo wa kupata elimu katika taifa hilo la Afrika magharibi ambapo mwaka jana ni watoto milioni 10.5 walioripotiwa kuathirika.

Rahama Farah, Mkuu wa UNICEF katika jimbo la Kano nchini humo ameeleza kuwa idadi hii kubwa ya watoto wasiokuwa shuleni imechangiwa na mashambulio yanyotekelezwa na makundi ya watu wenye silaha kaskazini mwa Nigeria, baadhi ya makundi hayo yakiwateka wanafunzi.

Tangu wapiganji wa Boko Haram kuwateka zaidi ya wanafunzi 200 kutoka shule moja ya wasichana  kaskazini mashariki wa Nigeria mwaka jana, watu wenye silaha wameripotiwa kuwateka karibia wanafunzi 1,500, UNICEF ikisema wanafunzi 16 waliripotiwa kufariki wakati wa matukio hayo ya utekaji.

Baadhi ya watoto waliokuwa wanazuiwa na wanajihadi tayari wameripotiwa kuaachiwa huru baada ya mazungumzo baina ya watekaji na wazazi wao ila bado wengine wanaendelea kushikiliwa na watekaji hao msituni.

Tangu Disemba 2020 zaidi ya shule 11,000 zimeripotiwa kufungwa nchini Nigeria kutokana na mashambulio ya makundi ya kijahadi yanyaoendeleza oparesheni zake kaskazini mwa taifa hilo, wazazi wakieleza hofu ya kuwapeleka wanao shuleni.

UNICEF imeonya kutokea kwa ndoa na mimba za mapema kutokana Kutokana na kufungwa kwa shule kasakzini mwa Nigeria kwa hofu ya kuvamiwa na magenge ya watu wenye silaha.

Mataifa ya Nigeria, Niger na Burkina Faso kwa muda sasa yamekuwa yakitatatizwa na makundi ya watu wenye silaha .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.