Pata taarifa kuu

Kenya: Odinga kukabidhiwa orodha ya wagombea wenza siku ya alhamis.

Nchini Kenya Jopokazi lilopewa jukumu la kuwapiga msasa watu wanaotaka kuwa wagombea wenza wa mgombea wa urais kupitia tiketi ya Azimio-One Kenya, Raila Odinga umetangaza kuhairisha shughuli ya kuwasilisha majina ya watu waliopendekezwa na jopo hilo kuwa wagombea wenza wa Odinga hadi alhamis ya mei 12.

Raila Odinga ,Mgombea urais nchini Kenya.
Raila Odinga ,Mgombea urais nchini Kenya. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Majina hayo yalifaa kuwasilishwa kwa kinara wa muungano huo Raila Odinga ambaye kwa mujibu wa mwenyekiti wa jop hilo Noah Wekesa yuko nje ya jiji kuu Nairobi kwa Shuguli za kutafuta kura ndio maana wameamua kusongeza mbele  shughuli hiyo iliyokuwa imepangwa kufanyika jumatano mei 11.

Jopo hilo litapendekeza majina ya watu watu kwa Odinga ambaye atakuwa na jukumu la kumchagua mtu anayemtaka kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa agosti 9.

Kiongozi wa chama cha Wiper  Kalonzo Musyoka, Sabina Chege  wa chama tawala cha (Jubilee), Martha Karua (NARC Kenya), Charity Ngilu (NARC), Peter Kenneth wa (  Jubilee ) Ali Hassan Joho (ODM) na  Stephen Tarus (National Liberal Party) wakiwa miongoni wa waliofika mbele ya kamati hiyo ya watu 7.

Waziri wa kilimo nchini humo Peter Munya, naibu kiongozi wa chama cha ODM kinachoongozwa na Odinga, Wycliffe Ambetsa Oparanya pamoja na gavana wa kaunti ya Nakuru Lee Kinyanjui wakiwa miongoni mwa watu 11 waliopigwa msasa kuwa wagombea wenza wa Raila.

Kwa upande mwengine aliyewahi kuhudumu kwa wakati moja kama gavana wa jimbo la kakamega , magharibi mwa kenya Boni Khalwale, anayegemea mrengo wake naibu rais William Ruto wa Kenya kwanza akizungumza wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha runinga kwenye taifa hilo la Afrika mashariki ameeleza kuwa  swala la mgombea mwenza tayari limeaafikiwa na kusuluhiswa katika mrengo wao.

Mrengo wa Ruto unajumuisha vyama 15 vikiwemo UDA chake naibu huyo wa rais, Ford kenya chake Moses Wetangula aliyewahi kuhudumu katika nafasi ya wizara ya mambo ya kigeni pamoja na ANC chake Musalia Mudavadi waziri wa zamani wa fedha.

Wagombea urais wanahadi Mei 16 kuwa wamewasilisha majina ya wagombea wenza wao kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini kenya (IEBC).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.