Pata taarifa kuu

Changamoto ya uteuzi wa wagombea wenza katika mrengo wa Azimio nchini Kenya.

Japokazi lilopewa majukumu ya kuwapiga msasa wanasiasa wanaotaka kuwa wagombea wenza wa mwaniaji wa urais kupitia tiketi ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya alliance Raila Odinga, linatarajiwa kukamilisha shughuli hiyo siku ya jumanne ya wiki hii.

Raila Odinga, Mgombea urais nchini Kenya.
Raila Odinga, Mgombea urais nchini Kenya. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Kamati hiyo yenye watu 7 chini ya uwenyekiti wa mbunge wa zamani Noah Wekesa, tayari imewapiga msasa watu kadhaa walionyesha nia ya kuwa wagombea wenza wa Odinga.

Miongoni mwa waliopigwa msasa hadi sasa ni mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Muranga Sabina Chege, gavana wa Kakamega ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa chama cha ODM Wyicliffe Oparanya, waziri wa zamani wa mambo ya haki na sheria Martha Karua, Ali Hassan Joho gavana wa Mombasa, waziri wa kilimo Peter Munya pamoja Peter keneth miongoni mwa mwengine.

Kiongozi wa chama cha KANU, Gideon Moi ambaye ni   mwanawe wa kiume wa rais wa zamani kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki Daniel Moi, hakufika mbele ya japokazi hilo , Moi badala yake akiaamua kumuunga mkono Kalonzo Musyoka  aliyekuwa kwa wakati moja naibu wa rais katika serikali ya rais wa zamani hayati mwai kibaki .

Kalonzo anatarajiwa kufika mbele ya jopokazi leo siku ya jummane japokuwa awali alikuwa amesisitiza kuwa hataenda kuhojiwa kutokana na tajiriba yake na kuwa yeye ndiye mtu anayefaa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Odinga.

Musyoka, ameendelea kusisitiza iwapo Odinga hatamteua kuwa mgombea mwenza wake kupitia tiketi ya Azimio la Umoja basi uwezekano wake wa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwezi agosti utakuwa finyu.

Zoezi hilo la kuwapiga msasa wanaotaka kuwa wagombea wenza wa Odinga liliaanza siku ya jumatano ya tarehe 4 ya mwezi huu ambapo linakamilika leo jumanne ya tarehe 10 mwezi huu.

Baada ya shughuli hiyo, Odinga anatarajiwa kupokezwa majina ya watu waliopendekezwa kugombea naye urais ambapo kwa mujibu wa jopokazi hilo atakuwa na uwamuzi wa mwisho wa kumteua anayependezwa naye.

Tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, (IEBC) imetoa makatta ya hadi mei 16 kwa wagombea wa urais kwenye taifa hilo kuwa wamewateua wagombea wenza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi agosti 9 mwaka huu wa 2022.

Ikumbukwe kuwa kalonzo alikuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa mwaka 2013, na 2017 kupitia muungano wa NASA ambapo amewahi kuwa naibu rais kwa wakati moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.