Pata taarifa kuu
NIGERIA

Ndege za abiria wa ndani kwa ndani kusitisha huduma zake nchini Nigeria.

Usafiri wa ndege za ndani kwa ndani unatarajiwa kutatizika nchini Nigeria baada ya Mashirika ya ndege kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi kutangaza kuwa yatasitisha huduma zake siku ya jumatatu ikiwa ni njia moja ya kuonyesha kughadhabishwa kwao na ogezeko la bei ya mafuta ya ndege.

Kituo cha mafuta jijini Lagos nchini Nigeria.
Kituo cha mafuta jijini Lagos nchini Nigeria. AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa wahudumu wa ndege za usafiri wa ndani kwa ndani nchini Nigeria (AON), katika taarifa yake, umeeleza kuwa bei ya mafuta imeongezeka mara nne mwaka huu peke hatua ambao muungano huo unasema imekuwa changamoto kwa kuendeleza baishara yao.

Ongezeko hili la bei ya mafuta ya ndege nchini humo, imehusishwa pakubwa na hatua ya Urusi kuishambulia Ukraine mwishoni mwa mwezi februari.

Tangu mwezi machi, kumeshuhudiwa ongezeko la kusitishwa na kucheleweshwa kwa safari za ndege nchini humo swala ambalo limehusihwa pakubwa na upungufu wa mafuta ya ndege, bei ya tiketi nazo pia zikipanda maradufu katika kipindi cha majuma kadhaa yaliopita.

Abiria nchini Nigeria wamekuwa wakilipa nauli kwa naira, pesa za nchini humo sarafu ambayo thamani yake imeendelea kushuka japokuwa wasamabazaji wa mafuta wanahitajika kulipwa kwa dolla za Marekani.

Licha ya Nigeria kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta barani Afrika, Nigeria inanunua mafuta yake ya ndege kutoka kwa mataifa ya kigeni.

Uhaba huu wa mafuta ya ndege unatarajiwa kuwaathiri pakubwa raia nchini humo wanaokabiliwa na changamoto kadhaa, Nigeria pia inakumbwa na tatizo la kuisalama ,wapiganaji wa kundi la Boko Haram wakitajwa kuwa hatari kwa usalama wa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.