Pata taarifa kuu

Guinea yaendelea kukumbwa na sintofahmu baada ya jeshi kuchukua madaraka

Viongozi wa kisiasa nchini Guinea, wamekerwa na hatua ya uongozi wa kijeshi nchini humo kwa kuwa na masharti magumu kwa jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, katika mchakato wa kurejesha utawala wa kiraia. 

Gari la kijeshi liliegeshwa mjini Conakry mnamo Septemba 14, 2021, siku chache baada ya mapinduzi nchini Guinea.
Gari la kijeshi liliegeshwa mjini Conakry mnamo Septemba 14, 2021, siku chache baada ya mapinduzi nchini Guinea. © JOHN WESSELS/AFP
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa kijeshi nchini Guinea, umejikuta katika mvutano na ECOWAS, ambayo imetoa muda mpaka Jumatatu kwa viongozi hao, kuwasilisha ratiba inayokubalika inayoeleza ni lini uongozi wa kiraia utarejeshwa nchini humo. 

 

 

Jumuiya ya ECOWAS, imeonya kuwa, iwapo uongozi wa kijeshi hautatoa ratiba inayoeleza mchakato huo, itawekewa vikwazo vya kiuchumi. 

Siku ya Jumatatu msemaji wa uongozi wa kijeshi Ousmane Gaoual Diallo alisema kuwa, kiongozi wa nchi hiyo Kanali Mamady Doumbouya hajatilia maanani wito huo wa ECOWAS. 

Mmoja wa viongozi wa kisiasa nchini humo Saikou Barry amesema iwapo ECOWAS, itaiwekea nchi hiyo vikwazo, wananchi wa Guinea ndio watakaoteseka, huku akiongeza kuwa, nchi hiyo haitaondoka kwenye jumuiya hiyo ya nchi za Afrika Magharibi. 

Mapinduzi ya kijeshi yalitokea nchini Guinea mwezi Septemba mwaka 2021 lakini haikuwekewa vikwazo kama ilivyokuwa kwa nchi ya Mali na Burkina Faso. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.