Pata taarifa kuu

Wanajeshi wawili wa Nigeria wafariki katika ajali ya ndege

Wanajeshi wawili waliokuwa wakiendesha ndege ya mafunzo walifariki dunia wakati ndege yao ilipoanguka huko Kaduna, kaskazini-magharibi mwa Nigeria siku ya Jumanne, msemaji wa jeshi la anga amesema siku ya Jumatano.

Jeshi la Nigeria, ambalo halina ufadhili wa kutosha na linaloshutumiwa kwa usimamizi mbaya, pia limekuwa likipambana na waasi wa kijihadi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 2009, mzozo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na milioni mbili kukimbia makazi yao.
Jeshi la Nigeria, ambalo halina ufadhili wa kutosha na linaloshutumiwa kwa usimamizi mbaya, pia limekuwa likipambana na waasi wa kijihadi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 2009, mzozo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na milioni mbili kukimbia makazi yao. REUTERS - Reuters Photographer
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Jeshi la Wanahewa Marshal Oladayo Amao alitembelea Kaduna "mapema leo ili kueleza mshikamano na familia, marafiki na wanajeshi wenzao wa marubani hao wawili (...) waliopoteza maisha katika ajali hii mbaya," msemaji wa jeshi Edward Gabkwet amesema katika taarifa.

Jeshi la Wanahewa la Nigeria litafanya "uchunguzi wa kina kuhusu sababu za kuanguka kwa ndege ya wakufunzi ya Super Mushshak", ameongeza, akimnukuu Field Marshal Amao.

Ndege kadhaa za kijeshi zimeanguka katika miaka ya hivi karibuni nchini Nigeria, nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika na inayokumbwa na machafuko mengi. Kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria ni eneo yanakofanyia uhalifu wao magenge ya wahalifu wanaofanya mashambulizi, kupora na kuwateka nyara wanavijiji, kuiba ng'ombe wao na kuchoma nyumba zao.

Mnamo Julai 2021, jeshi lilitangaza kwamba moja ya ndege zake za kivita ilianguka baada ya kutunguliwa na "majambazi" katika jimbo la Zamfara (kaskazini magharibi). Rubani alifanikiwa kuondoka kabla ya kuokolewa. Miezi miwili mapema, mwezi Mei, maafisa 11, akiwemo mkuu wa jeshi wakati huo Jenerali Ibrahim Attahiru, waliuawa wakati ndege yao ilipoanguka kufuatia hali mbaya ya hewa katika jimbo la Kaduna.

Rais Muhammadu Buhari, jenerali wa zamani wa jeshi madarakani tangu mwaka 2015, anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kushindwa kutoa usalama kwa watu wanaokadiriwa kuwa milioni 215.

Jeshi la Nigeria, ambalo halina ufadhili wa kutosha na linaloshutumiwa kwa usimamizi mbaya, pia limekuwa likipambana na waasi wa kijihadi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 2009, mzozo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na milioni mbili kukimbia makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.