Pata taarifa kuu

CAR: Kesi ya kwanza ya Mahakama Maalum ya Jinai

Kesi ya kwanza ya Mahakama Maalumu ya Jinai nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (SCC), inayoundwa na majaji kutoka nchini humo na nchi za kigeni wanaohusika na kushughulikia uhalifu wa kivita, iliyokuwa ianze kusikilizwa Jumanne huko Bangui, imeahirishwa hadi Aprili 25 kutokana na kutokuwepo kwa mawakili wa upande wa utetezi.

Mahakama Maalum ya Jinai katika ufunguzi wa kesi ya kwanza mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Aprili 19, 2022.
Mahakama Maalum ya Jinai katika ufunguzi wa kesi ya kwanza mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Aprili 19, 2022. © RFI/Carol Valade
Matangazo ya kibiashara

SCC ingewasikiliza na kuwahukumu kuanzia Jumanne wiki hii wanamgambo watatu wa moja ya makundi yenye nguvu zaidi yenye silaha ambayo yametishia maisha ya raia kwa miaka kadhaa. Wanamgambo hao ambao ni Issa Sallet Adoum, Ousman Yaouba na Tahir Mahamat kutoka kundi la 3Rswanashtumiwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Wanaume hao watatu wanatuhumiwa kwa mauaji ya Mei 2019 ya raia 46 katika vijiji vya kaskazini-magharibi mwa nchi. Mara tu kesi ilipoanza kusikilizwa, Aimé-Pascal Delimo, jaji mkuu wa SCC amebainisha "kutokuwepo" kwa mawakili wa upande wa utetezi. "Tunaahirisha kusikilizwa kwa kesi hii hadi Aprili 25," amesema.

"Mwanzo huu wa kesi unaonyesha kwamba utendakazi wa CPS unasalia kuwa mgumu licha ya kuungwa mkono na wafadhili wa kimataifa," Enrica Picco, mkurugenzi wa mradi wa Afrika ya Kati katika shirika la Kimataifa linalohusika na kutatua Migogoro (ICG) ameliambia shirika la habari la AFP.

Hivi karibuni shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch lilisema kuanza kesi ya kwanza kwenye Mahakama Maalum ya Uhalifu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (SCC) ni mwanzo wa kusaka haki ya wahanga wa uhalifu wa kivita nchini humo.

Wakili wa ngazi za juu wa sheria za kimataifa katika Human Rights Watch, Esti Tambay, alisema kesi hii ya kwanza na hatua muhimu kwa wahanga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wamekuwa wapigania haki kutendeka dhidi ya uhalifu wa kinyama uliontendeka wakati wa migogoro iliyofululiza nchini humo.

Mahakama hiyo Maalum ya Uhalifu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (SCC) ilianza kazi rasmi mwaka 2018 ili kusaidia kuzuwia kiwango kikubwa cha hali ya wakosaji kutochukuliwa hatua kwa makosa makubwa ya uhalifu nchini humo.

Mahakama hiyo ina majaji na waendesha mashitaka wa ndani na wa kimataifa na gharama zake hulipwa na msaada wa kimataifa.

Ina mamlaka ya kutoa hukumu kwa makosa ya uhalifu mkubwa uliotendeka wakati wa mapigano yaliyoanza tangu mwaka 2003.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.