Pata taarifa kuu

Uturuki na DRC zakubali kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya ziara ya kihistoria nchini DRC tangu Jumapili Februari 20 kwa lengo la kuimarisha uhusiano na nchi hiyo katika nyanja mbali mbali ikiwemo usalama na biashara.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi alimpokea Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu ya rais huko Gombe mnamo Februari 20, 2022.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi alimpokea Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu ya rais huko Gombe mnamo Februari 20, 2022. AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zimetia saini mikataba, katika nyanja za uchumi na usalama. Makubaliano yaliyotiwa saini wakati wa ziara ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan nchini DRC. Rais wa Uturuki akiambatana na mkewe waliwasili mjini Kinshasa Jumapili hii, wakiongozwa na ujumbe mkubwa kutoka nchi hiyo.

Rais wa Uturuki na mwenyeji wake wa DRC Félix Tshisekedi walitia saini kwenye mikataba mbalimbali katika nyanja ya usalama na vile vile ya afya, miundombinu na uchukuzi. Bila kutoa maelezo zaidi, Rais Félix Tshisekedi, ambaye amezungumza mwishoni mwa kikao, amesema ameridhishwa na ushirikiano huu wa pande mbili.

Pamoja na mengine rais Tschisekedi amesema Kongo na Uturuki zimefikia makubaliano ya manufaa kwa pande zote mbili ambayo yatajenga ushirikiano kuhusu masuala ya usalama, miundombinu, afya pamoja na uchukuzi,lakini juu ya hilo rais huyo wa Kongo akaitaja jana kuwa ni siku ya kihistoria katika uhusiano kati mataifa hayo mawili baada ya kuzungumza na Erdogan.

Mnamo mwezi Septemba,rais Tshisekedi alifanya ziara rasmi mjini Ankara,Uturuki akiwa na agenda ya kutafuta ushirikiano wa kiuchumi na nchi hiyo lakini pia alikwenda Istanbul mwezi Desemba mwaka jana alikoshiriki mkutano wa kilele baina ya Uturuki na Afrika.

Uhusiano baina ya Ankara na Kinshasa ni mzuri kwa kipindi cha miaka mingi na kiwango cha uwekezaji wa Uturuki nchini Kongo umeendelea kuongezeka.

Ziara hii ya Erdogan barani Afrika iliyoanza jana tarehe 20 mpaka 23  haishii tu nchini Kongo bali itamfikisha pia Senegal  na Guinea Bissau.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.