Pata taarifa kuu

Chad: Kiongozi wa waasi wa UFR kushirkiana na kundi la mamluki la Wagner

Katika sauti iliyorekodiwa na ambayo imethibitishwa na vyanzo kadhaa, kiongozi wa kundi la waasi la UFR nchini Chad, Timan Erdimi anasikika akizungumza na waziri mshauri maalum wa rais wa Afrika ya Kati, Aboulkhassim Algoni Tidjani.

Kiongozi wa waasi Timan Erdimi.
Kiongozi wa waasi Timan Erdimi. (Photo : Laurent Correau/ RFI)
Matangazo ya kibiashara

Katiika sauti hiyoanasikika akieleza nia yake ya kulishawishi kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, wanaofanya kazi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanafanya kazi pamoja na serikali ya nchi hii, ili kumsaidia "kumuondoa mamlakani rais wa Kamati ya Mpito ya Kijeshi, anayeshikilia madaraka” nchini Chad, Mahamat Idriss Déby.

Nani amevujisha waraka huu wa sauti kwenye mitandao ya kijamii kwa siku chache? Kwa nini? Maswali mengi bado hayajajibiwa hadi sasa.

Katika rekodi hiyo, kiongozi huyu wa waasi pia anazungumzia kuhusu mawasiliano yake na Waziri wa Kilimo wa Afrika ya Kati, na hata kumtangazia kwamba alikuwa amejaribu bila mafanikio kukuta na Rais Michel-Archange Touadéra ambaye wakati huo alikuwa ameshirikia katika mkutano wa Umoja wa Afrika, ambao ulifanyika siku kumi zilizopita mjini Addis Ababa.

"Shetani"

Kwa upande wa serikali ya Chad wanasema, hakuna suala la kukaa meza moja na Timan Erdimi, ambaye anataka kufanya mapatano na kundi la Wagner, huku ikilitaja kundi hilo kuwa ni "shetani". Serikali ya Chad imebaini kwamba kiongozi wa UFR alijiondoa kwenye mazungumzo ya awali ya Doha. "Kwa kisingizio kwamba anataka kuifukuza Ufaransa, anataka kulifukuza Baraza la Mpito la Kijeshi. Lakini ikiwa Timan Erdimi anaweza kwenda kufanya mapatano na shetani ili aje kuchochea uhasama, aje ahatarishe usalama nchini, hilo ni jambo zito sana. Hatutakubali kwamba mtu huyu anayepanga kuingia vitani wakati ambapo watu wanataka amani anaweza kuhudhuria vikao vya kabla ya mazungumzo,” msemaji wa serikali Abderaman Koulamallah, amesema.

Kwa hili, anategemea kamati maalum ya kiufundi na Qatar, yenye jukumu la kuandaa mazungumzo ya awali na makundi yenye silaha ya Chad yaliyopangwa kufanyika kwa siku kadhaa huko Doha.

Serikali ya Chad pia inaashiria uhusiano kati ya Timan Erdimi na mshauri maalum wa rais wa Afrika ya Kati ambaye pia ni Waziri wa Kilimo. Inashangaa kumuona akiwa na nambari ya simu ya Faustin-Archange Touadéra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.