Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Shambulio la wanajihadi laua watu wanajeshi wawili wa Mali

Wanajeshi wawili wa Mali waliuawa mapema Jumapili kaskazini mwa Mali katika shambulio dhidi ya ngome yao, shambulio linalohusishwa kundi la wanajihadi, jeshi limetangaza kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanajeshi wa jeshi la Mali.
Mwanajeshi wa jeshi la Mali. 9. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Ngome ya Niafunke ilishambuliwa mwendo wa saa nane usiku na "kundi la kigaidi lililokuwa limejihami kwa silaha za kivita", jeshi limesema, likitumia neno la wanajihadi.

"Idadi ni ya watu wawili waliouawa kwa upande wa FAMa (Jeshi la Mali) na watano waliuawa kwa upande wa washambuliaji," jeshi limeongeza.

Wakati huo huo, jeshi la Mali limedai kuhusika na vifo vya makumi ya wanajihadi na kuharibu kambi zao kadhaa tangu kuzinduliwa kwa operesheni inayoitwa Kèlètigui, mwezi Desemba.

Tangu mwaka 2012, wanajihadi wamesababisha vifo vya mamia ya maafisa wa vikosi vya usalama vya taifa nchini Mali na majirani zake Burkina Faso na Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.