Pata taarifa kuu

EU yaahidi kuipa Afrika zaidi ya euro bilioni 150 katika uwekezaji

Rais wa Tume ya Ulaya anazuru Dakar, Senegal. Ursula von der Leyen alipokelewa Alhamisi hii, Februari 10 na Rais wa Senegal, Macky Sall, Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika. Kulikuwa na mazungumzo ya mkutano ujao wa kilele wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya (AU/EU), ambao utafanyika Brussels tarehe 17 na 18 Februari. Ursula von der Leyen pia alitangaza mpango mkubwa wa uwekezaji kwa bara la Afrika.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Senegal Macky Sall wakati wa ziara yake huko Dakar mnamo Februari 10, 2022.
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Senegal Macky Sall wakati wa ziara yake huko Dakar mnamo Februari 10, 2022. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

"Ulaya na Afrika zina nia ya kufanya kazi pamoja," rais wa Senegal alisema katika taarifa ya pamoja. Kwa upande wake, Ursula von der Leyen alitangaza mpango wa kikanda wa euro bilioni 150 za uwekezaji barani Afrika, kama sehemu ya mkakati wake mpya wa uwekezaji unaoitwa "Global Gateway".

“Leo, ninajivunia kutangaza zaidi ya euro bilioni 150 kupitia mpango wa Afrika-Ulaya; ni mpango wa kwanza kabisa wa kikanda chini ya Global Gateway,” aliambia wanahabari, akimaanisha mpango wa Ulaya uliozinduliwa mwezi Desemba mwaka jana.

Global Gateway inatarajia kukusanya hadi euro bilioni 300 katika fedha za umma na za kibinafsi ifikapo 2027, katika miradi ya miundombinu kote ulimwenguni. Pesa hizo zitaenda kwa nishati mbadala, kupunguza hatari ya majanga ya asili, Waafrika kuingia kiurahisi kwenye mitandao ya intaneti, usafiri, uzalishaji wa chanjo au elimu, waraka unasema.

"Kwa haya yote, bila shaka tunahitaji sekta ya kibinafsi, kwa utaalamu wake na uwekezaji wake imara, pia tunahitaji kujitolea kwa kisiasa katika ngazi ya juu," alitangaza Ursula von der Leyen, pamoja na Rais wa Senegal Macky Sall.

Ziara ya rais wa Tume ya Ulaya inatanguliza mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika wa Februari 17 na 18 huko Brussels.

"Uwekezaji utakuwa kiini cha majadiliano" ya mkutano huu, alisisitiza Bi. von der Leyen. "Katika sekta hii, Ulaya ni mshirika wa kutegemewa zaidi kwa Afrika na kwa kiasi kikubwa ndio muhimu zaidi," aliongeza. Rais wa Tume ya Ulaya alikariri kuwa Global Gateway ilizingatia "maadili ambayo Ulaya na Afrika zimeshikamana, kama vile uwazi, uendelevu, utawala bora na kujali ustawi wa watu".

Global Gateway inaonekana kama jibu kwa Barabara mpya za hariri za China. Barani Afrika pia, China inapanua kwa kasi uwepo wake wa kiuchumi na kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.