Pata taarifa kuu
NIGER-HAKI

Niger: Vigogo wanane katika utawala wa Habyarimana kurudishwa Arusha

Wanyarwanda wanane waliotumwa Niger, mwanzoni mwa mwezi Desemba, Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wanapaswa kurejeshwa walikotoka mjini Arusha, nchini Tanzania.

Ofisi za Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda mjini Arusha.
Ofisi za Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda mjini Arusha. (CC)/Tomsudani/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Maafisa hao katika utawala wa Juvénal Habyarimana, wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, ambao baadhi walikutwa bila hatia na wengine kuachiliwa huru na ICTR baada ya kumaliza kifungo chao, wanapaswa kurejeshwa Arusha. Angalau ndivyo anavyoamuru mmoja wa majaji wa mahakama ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Rwanda-'International Residual Mechanism for Criminal Tribunals' (IRMCT) mjini Hague - mahakama inayosikiliza kesi za uhalifu wa vita za Rwanda na iliyokuwa Yugoslavia.

"Suluhu la muda", anasisitiza amebaini Jaji. Tanzania, ambapo kunapatikanaMahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa, italazimika tena kuwapokea Wanyarwandahao wanane. "Suluhisho lisilo kamili" ameandika jaji katika uamuzi wake kwa "tatizo lisiloweza kutatuliwa".

Waliokuwa maafisa wakuu na mawaziri wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, wamekuwa wakisubiri kwa zaidi ya miaka 15 kupata hifadhi, katika baadhi ya nchi kama vile Ufaransa, Ubelgiji, Canada au hata Denmark, ambako zinaishi sehemu ya familia zao. Lakini nchi hizi zilikataa kuwawapokea, hali ambayo inasumbuwa Umoja wa Mataifa.

Katika makubaliano yaliyotiwa saini katikati ya mwezi Novemba, Niamey ilikuwa imeyakubali. Lakini mwishoni mwa mwezi Desemba, wakiwa na makazi mapya nchini Niger, maafisa hao wanane walipokea taarifa ya kufukuzwa kutokana na "sababu za kidiplomasia". Rwanda ilitangaza kutofurahishwa na uamuzi wa Niger wa kuwapokea watu hao.

Kwa mujibu wa jaji kiongozi, kurudi kwao mjini Kigali, jambo ambalo kila mtu anapinga, haliwezi kufanywa bila ridhaa yao au bila kuwasikiliza.

Jaji huyo anaishutumu Niger kwa "ukiukaji wa wazi" wa makubaliano na uwezekano wa ukiukaji wa haki za watu hao wanane. ameikosoa Niamey kwa kudokeza kwamba neno la Umoja wa Mataifa litakuwa kama "janja tu ya kuwahadaa watu binafsi".

Hakuna tarehe iliyopangwa ya kuwarudisha watu hao wanane mjini Arusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.