Pata taarifa kuu

Mtandao wa Twitter warudi tena kufanya kazi Nigeria

Serikali ya Nigeria, imeondoa marufuku ya mtandao ya Twitter, miezi saba baada ya kuizua, kwa kuufuta ujumbe wa rais Muhammadu Buhari kuhusu kuwachukulia hatua wanaharakati wanaoshinikiza kujitenga.

Serikali ya Nigeria inasema imeamua kuondoa marufuku hayo, baada ya Twitter kukubali kusajili huduma zake nchini humo ndani ya miezi mitatu ijayo, kumteua mwakilishi wake nchini humo, kulipa kodi na kutii sheria za nchi hiyo.
Serikali ya Nigeria inasema imeamua kuondoa marufuku hayo, baada ya Twitter kukubali kusajili huduma zake nchini humo ndani ya miezi mitatu ijayo, kumteua mwakilishi wake nchini humo, kulipa kodi na kutii sheria za nchi hiyo. AP - Matt Rourke
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Juni mwaka uliopita, serikali ya Nigeria ilichukua hatua hiyo kwa kile ilichosema Twitter ilikuwa inaunga mkono harakati za wanaharakati wanaotaka kujitenga.

Twitter kwa upande wake, ilisema ilichukua hatua hiyo baada ya ujumbe wa rais Buhari, kuvunja kanuni zake.

Serikali ya Nigeria inasema imeamua kuondoa marufuku hayo, baada ya Twitter kukubali kusajili huduma zake nchini humo ndani ya miezi mitatu ijayo, kumteua mwakilishi wake nchini humo, kulipa kodi na kutii sheria za nchi hiyo.

Hata hivyo, Twitter haijasema iwapo imekubaliana na masharti hayo ya Nigeria, lakini imeeleza kwenye ukursa wake kuwa, imefurahi kurejea nchini humo.

Kabla ya hatua hii ya serikali ya Nigeria, watu nchini humo wamekuwa wakitumia mtandano wa kibifasi wa VPN kwa ajili ya mawasiliano huku wachambuzu wakisema, kwa kipindi cha mieizi saba iliyopita, wafanyibiashara wamepata  hasara ya mamilioni ya Dola kwa kushindwa kuwasiliana na wateja wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.