Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA

Shambulizi la Kouré nchini Niger: Mmoja wa wahusika wakuu auawa

Jeshi la Ufaransa limetangaza kumuua mmoja wa wahusika wa wakuu wa mauaji ya wafanyakazi sita wa mashirika ya kibinadamu kutoka Ufaransa na wenzao wa Niger katika hifadhi ya Kouré Agosti 2020. Mtu huyo ametajawa kama mwanachama wa kundi la Islamic State katika ukanda wa Grand Sahara (EIGS).

Mabaki ya gari lililokuwa limewabeba Wafaransa 6 na Waniger 2, waliouawa katika shambulio la Jumapili, Agosti 9, 2020, katika eneo la Kouré, kusini-mashariki mwa Niamey, mji mkuu wa Niger.
Mabaki ya gari lililokuwa limewabeba Wafaransa 6 na Waniger 2, waliouawa katika shambulio la Jumapili, Agosti 9, 2020, katika eneo la Kouré, kusini-mashariki mwa Niamey, mji mkuu wa Niger. Boureima HAMA AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Soumana Boura aliuawa siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Ufaransa. Makao makuu ya jeshi la Ufaransa yamemtambua kama anaongoza kundi la wapiganaji kadhaa wa EIGS katika maeneo ya Gober Gourou na Firo magharibi mwa Niger. Anachukuliwa kuwa mmoja wa wahusika wa kuu wa kundi lililowaua wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada kutoka Ufaransa, mwongozaji na dereva wao, raia wa Niger, katika hifadhi ya twiga ya Kouré, yapata kilomita sitini kutoka Niamey, mji mkuu wa Niger Agosti 2020. Kisha alirekodi tukio hilo la mauaji na kulirusha kwenye mitandao ya kijamii.

Mashambulizi ya anga

Kulingana na taarifa, Soumana Boura aliuawa siku ya Jumatatu, katika eneo la Tillabéri, ambalo lilikuwa eneo lake la kawaida kwa kuishi. Alishambuliwa na ndege isio na rubani wakati alikuwa peke yake kwenye pikipiki. Operesheni iliyofanywa kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka ya Niger, kulingana na makao makuu ya jeshi la Ufaransa, ambayo pia yanabainisha kuwa kitengo cha wanajeshi wa ardhini wa Ufaransa kilitumwa kupekua eneo hilo na kumtambua rasmi mwanajihadi huyo.

Watu kadhaa wakamatwa nchini Niger

Mauaji ya Kouré yalidaiwa mwezi mmoja baadaye na kundi la Islamic State. Mwezi wa Agosti mwaka huu, Paris ilitangaza kuwa ilimuua kiongozi wa kundi la EIGS, Adnan Abou Walid al Sahraoui, ambaye aliamuru shambulio hilo. Watu kadhaa wanaohusiana na kesi hii pia walikamatwa nchini Niger katika miezi ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.